Mtandao wa 5G wazinduliwa kwa mara ya kwanza Tanzania

September 1, 2022 12:58 pm · Nuzulack Dausen
Share
Tweet
Copy Link
  • Watanzania watapata huduma hiyo kupitia kampuni ya Vodocom.
  • Teknolojia hiyo inatoa kasi ya hali ya juu ya intaneti.
  • Itarahisha shughuli ikiwemo biashara zinazofanyika mtandaoni. 

Dar es Salaam. Kwa mara ya kwanza, Watanzania sasa watapata fursa ya kutumia teknolojia ya mawasiliano ya 5G baada ya kampuni ya Vodacom kuzindua huduma hiyo ikiwa ni miongoni mwa mataifa ya mwanzo kabisa Afrika. 

5G itawawezesha watumiaji kupata intaneti ya kasi zaidi ambayo pamoja na mambo mengine inawezesha kuwasiliana kwa video kupitia teknolojia ya hologram.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Hilda Bujiku amesema hii ni mara ya kwanza Tanzania itakuwa na mawasiliano ya 5G ikiwa ni jitihada za kuongeza fursa zaidi za kiuchumi kupitia dijitali.

5G ni moja ya teknolojia inayokua kwa kasi duniani na Afrika. Baadhi ya nchi ambazo zimeshaanza kutumia ni Kenya, Misri, Afrika Kusini, Uganda na nyinginezo.

Andrew Lupembe, Mkurugenzi wa Huduma za Mtandao wa Vodacom amesema wanatarajia huduma hiyo itaanza kupatikana katika baadhi ya mikoa kama Dar es Salaam, Njombe, Dodoma, Arusha, Mwanza na mingine kuanzia Novemba 2022. 

Kwa sasa huduma hiyo itaanza kupatikana kwa wateja ambao ni kampuni na vifaa vya intaneti kama Routers. 

“Uwepo wa teknolojia hii utasaidia katika kuongeza ufanisi viwandani kupitia dijitali (Industrial automation), masuala ya akili bandia (artificial intelligence), huduma za afya, usafirishaji na utalii,” amesema.


Soma zaidi: 


Katika hotuba yake, Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema mapema Mei mwaka huu walitangaza kuwa katika mwaka wa fedha wa 2022/23 Serikali itawezesha upatikanaji wa teknolojia ya 5G na hakutegemea jambo hilo lingefanikiwa ndani ya miezi mitatu.

“Ni matumaini yangu wengine (kampuni za mawasiliano) watafuata na watakuja kwa kasi…teknolojia mpya inayozinduliwa leo italeta matokeo chanya kiuchumi,” amesema Nape.

Kwa sasa, mtandao wa 4G ndiyo unatumika zaidi Tanzania na duniani lakini ujio wa 5G ni mapinduzi makubwa katika huduma za intaneti

5G ni njia rahisi na ya haraka ya kupakua na kuweka vitu mtandaoni. Inawezesha kuangalia video na kusikia sauti yenye kiwango kizuri pasipo kukwama kwama kwenye simu au kompyuta yako.   

Mtandao huo unapanua uwanja wa matumizi ya teknolojia hasa kwa wale wanaotumia mtandao kuendesha vyombo vya usafiri katika miji mikubwa duniani.

Ni mtandao wa kuaminika na kutegemewa katika simu za mkononi kutokana na kuwa rahisi katika kuunganisha vifaa vya IoT vinavyotuma data kwenda katika mtandao bila kuhusisha binadamu kwa binadamu au binadamu na kompyuta.

Enable Notifications OK No thanks