Nchi 6 kati ya 10 za kipato cha chini Afrika ziko kwenye mzigo wa madeni

October 4, 2022 6:27 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Ukosefu wa uwezo wa kifedha na kupata chanjo unakwamisha maendeleo ya uchumi wa nchi nyingi zinazoendelea. Picha | ILO/K.B. Mpofu.


  • UNCTAD imesema  takriban asilimia 60 ya nchi za kipato cha chini barani Afrika hivi sasa ziko kwenye mzigo wa madeni, shinikizo kubwa au katika hatari ya kuingia kwenye madeni.
  • Hali hiyo inaweza kuwatumbukiza mamilioni ya watu kwenye umaskini na njaa.

Dar es Salaam. Takriban nchi sita kati ya 10 za kipato cha chini barani Afrika ziko kwenye mzigo wa madeni, shinikizo kubwa au katika hatari ya kuingia kwenye madeni, jambo linaloweza kuwatumbukiza mamilioni ya watu kwenye umaskini, imeeleza ripoti mpya.

Ripoti mpya ya biashara na maendeleo kwa mwaka 2022 iliyotolewa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Biashara na Maendeleo (UNCTAD) imesema hali hiyo takriban asilimia 60 ya nchi za kipato cha chini barani Afrika hivi sasa ziko kwenye mzigo wa madeni, shinikizo kubwa au katika hatari ya kuingia kwenye madeni.

UNCTAD imesema kwa hali hiyo, mamilioni ya Waafrika wanaweza kutumbukia tena kwenye umasikini wakati huu wakiwa kwenye hatari kubwa ya kutokuwa na uhakika wa chakula.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyotolewa mjini Geneva Uswis, kiwango cha ukuaji uchumi cha Afrika mwaka huu wa 2022 kinatarajiwa kukua kwa asilimia 2.7 huku 2023 kikikuwa wa asilimia 2.4 ukilinganisha na ukuaji wa asilimia 5.1 uliokuwa mwaka 2021. 

“Na matokeo yake watu wengine milioni 58 barani Afrika watalazimika kutumbukia kwenye umasikini uliokithiri mwaka huu na kujiunga na wengine milioni 55 ambao tayari wako kwenye ufukara,” imeeleza ripoti hiyo. 

Katibu Mkuu wa UNCTAD Rebeca Grynspan amesema ”kuzorota huku kwa uchumi kunasababisha mkwamo wa kufikia agenda ya 2030 ya maendeleo endelevu. Na madeni yanazikabili sekta zote Afrika kuanzia za umma na sekta binafsi.” 

Mbali ya mzigo wa madeni ripoti hiyo ya UNCTAD imesema zaidi ya asilimia 60 ya nchi za Afrika zinahitaji msaada wa chakula kutoka nje wakati huu njaa ikisambaa haraka kwenye bara hilo. 

Kudorora huko kwa uchumi kunaleta changamoto zingine lukuki ikiwemo ongezeko kubwa la bei za mafuta na chakula, shinikizo katika sera za fedha kwa nchi zilizoendelea na hatari kubwa ya kutokuwa na uhakika wa chakula katika maeneo mengi ya kanda hiyo. 

Nchi tatu za Africa ambazo uchumi wake ndio unashikilia asilimia 60 ya pato la bara hilo Nigeria, Misri na Afrika Kusini ripoti hiyo imesema ukuaji wa uchumi umeshuka ikilinganishwa na mwaka 2021. 

“Shirika la fedha duniani (IMF) na Benki ya Dunia wameingilia kati kwa program maalum kuzisaidia nchi 16 za kipato cha chini Afrika zilizo na mzigo mkubwa wa madeni na zilizo katika hatari ya mzigo huo ili kupunguza mzingo huo zikiwemo Zambia, Ghana na Tunisia,” imeeleza ripoti hiyo.

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limekadiria kuwa nchi 33 za Afrika zinahitaji msaada wa chakula toka nje wakati  hali ya kutokuwa na uhakika wa chakula ikitarajiwa kuwa mbaya zaidi katika miezi 18 ijayo katika nchi hizo. 

“Kupanda kwa bei ya mbolea kwa sababu ya vita inayoendelea Ukraine kunatishia kupunguza uzalishaji wa chakula na kuongeza mgogoro wa chakula duniani huku wakulima wadogo wakiwa ndio waathirika zaidi. Hali ni mbaya zaidi hususan Mashariki na Magharibi mwa Afrika kutokana na uzalishaji mdogo wa kilimo , ukame, na migogoro”,. amesema Grynspan. 

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
26 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV