Hapana: Serikali haitakata pensheni za wastaafu kugharamia mfuko wa bima ya afya

October 12, 2022 3:52 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Waziri Ummy asema huo ni uzushi.

Dar es Salaam. Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema taarifa zinazosambaa mtandaoni kuhusu Serikali kukata pensheni za wastaafu kugharamia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), siyo za kweli.

Kumekuwa na taarifa ya uzushi inayosambaa mitandaoni inayodai kuwa Serikali itakata asilimia tano ya fedha za mafao ya uzeeni na kuzipeleka kwenye mfuko wa bima ya afya. 

Uzushi huo unaosambazwa kupitia ukurasa wa Twitter wa Tanzania Abroad Tv unadai kuwa Serikali imefikia uamuzi huo ili kufidia uhaba wa fedha uliopo kwenye mfuko huo.


Soma zaidi:


Waziri Ummy kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema taarifa hiyo haina ukweli wowote ni uzushi.

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na mjadala mpana kuhusu utendaji wa NHIF baada ya kuelemewa na madeni huku Serikali ikisisitiza mfuko huo utaendelea kutoa huduma.

Tayari, Serikali imewasilisha Bungeni muswada wa Bima ya Afya kwa Wote ambapo sheria yake ikipita utawawezesha Watanzania wengi kupata huduma za afya kwa uhakika.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
31 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
31 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV