Falme za kiarabu, Tanzania kuanza usambazaji wa kimkakati wa mbolea

February 25, 2023 11:43 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Falme za Kiarabu kujenga kituo maalum cha kuhifadhi na kusambaza mbolea kwa wakulima.
  • Kitasaidia kuwafikia wakulima kirahisi ili kuongeza uzalishaji. 

Dar es Salaam. Huenda uhaba wa mbolea unaowakumba wakulima wa Tanzania utapungua siku za hivi karibuni baada ya wawekezaji kuonyesha nia ya kuimarisha mfumo wa usambazaji pembejeo hiyo nchini. 

Ofisi ya Sheikh Ahmed Dalmook Al Maktoum, Mwanafamilia ya Kifalme ya Falme za Kiarabu (UAE) imetia saini mkataba wa makubaliano na Wizara ya Kilimo ili kuendesha usambazaji wa kimkakati na uhifadhi wa mbolea kwa ajili ya kuimarisha usalama wa chakula nchini.

Makubaliano hayo yaliyofanyika leo Februari 25, 2023 yanaonyesha utayari wa kutoa na kusambaza mbolea ya uhakika na yenye ubora kwa Tanzania ili kuchagiza sekta ya kilimo na kuboresha upatikanaji wa chakula kwa wananchi.

Kwa mujibu wa masharti ya makubaliano hayo, ofisi hiyo ya Sheikh Al Maktoum pamoja na washirika wake itaendeleza na kuendesha kituo cha kisasa cha kuhifadhi mbolea nchini Tanzania, ambacho kitakuwa na uwezo wa kufanya usambazaji wa kimkakati wa bidhaa za mbolea.

Jukumu la Serikali ya Tanzania litakuwa kuimarisha miundombinu iliyopo katika maeneo ambayo mbolea itakuwa inasambazwa ili kuwafikia wakulima kirahisi. 

Kituo hicho kitawekwa kimkakati ili kuhakikisha kuwa wakulima kote nchini wanapata mahitaji ya mbolea kwa bei shindani.

Ushirikiano huu utasaidia kuhakikisha wakulima wa Tanzania wanapata mbolea yenye ubora wa hali ya juu ambayo ni muhimu kwa ukuaji wa mazao na mafanikio ya sekta ya kilimo.

“Tuna furaha kubwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kusaidia sekta ya kilimo nchini,” amesema Sheikh Al Maktoum na kusisitiza kuwa,

“MOU (Makataba wa Makubaliano) hii inawakilisha hatua kubwa ya maendeleo katika juhudi zetu za kuwapatia wakulima nchini Tanzania mbolea yenye ubora wanayohitaji ili kukuza mazao yenye afya na kuboresha maisha yao.”

Ushirikiano huu wa kimkakati utasaidia kukuza ukuaji wa uchumi, kuboresha usalama wa chakula, na kukuza mazoea ya kilimo endelevu nchini. 

Ofisi Sheikh Al Maktoum  imedhamiria kufanya kazi kwa karibu na Serikali ya Tanzania ili kuhakikisha mpango huu unafanikiwa na inatarajia ushirikiano wa muda mrefu na wenye tija.

/
No matches found for this filter
31 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
31 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
31 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV