Siri iliyofichika watoto mapacha kuhusishwa na “mikosi” Kanda ya Ziwa-4

January 13, 2021 6:15 am · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Baadhi ya watu wanasema siyo sahihi kuwahusisha mapacha na mikosi kwa sababu watoto wote ni baraka kutoka kwa Mungu.
  • Wataalam wa afya wanaeleza kuwa suala la wanawake kuzaa mapacha ni la kibaolojia na halina mahusiano yoyote na mikosi.
  • Serikali yasema inaheshimi imani tofauti za watu ikiwa haziathiri haki za binadamu.

Mwanza. Licha ya kuwa Wakango wanaamini kuwa watoto mapacha lazima wafanyiwe tambiko ili kuwaondolea mikosi, wanajumuiya wengine wa kabila la Kisukuma, wataalamu wa afya, viongozi wa Serikali na dini wana mtazamo tofauti kuhusu mila hiyo.  

“Ni imani tu maana kuna watu wamezaa mapacha hawajafanya matambiko kama haya wanaishi vizuri tu hakuna magonjwa, vifo na mali wanazo, kwa hiyo kila mmoja anavyoamini,”anasema Rahel Cosmas mkazi wa kijiji cha Mwamajila.

Hata hivyo, ni muhimu kufahamu kuwa mila hiyo hufanywa na baadhi ya Wasukuma huku wengine hawaamini kuwa kuzaa mapacha ni laana. 

“Tunafanya matambiko siyo kwa ubaya isipokuwa ni kumkinga pacha mmoja asifariki lakini kiujumla kwetu mapacha ni baraka na si mkosi,” anasema Emanuel Shoto mkazi wa Wilaya ya Bariadi Mkoa wa Simiyu. 

Aliyekuwa Waziri wa Madini, Dotto Biteko ambaye ni pacha ameiambia Nukta (www.nukta.co.tz) kuwa yeye pamoja na ndugu yake Kulwa licha ya kuzaliwa usukumani hawakuwahi kufanyiwa matambiko yanayodaiwa kuondoa mikosi. 

Anabainisha kuwa hizo ni imani na zimegawanyika katika makundi mawili yaani kwa wanaoamini kuwa ni mkosi na wanaoamini kuwa ni baraka na wote huzitumia kwa faida zao wenyewe.

Wakango wakigawana Karanga na pipi kwenye sherehe za tambiko zilizofanyika katika kijiji cha Mwamajila wilayani Kwimba. Ugawanywaji wa karanga hizo ni moja ya shukrani ambazo familia inayofanyiwa tambiko hautoa ili iweze kubarikiwa. Picha|Mariam John. 

Ni tatizo la kiafya kuzaa mapacha?

Wataalam wa afya wanaeleza kuwa suala la wanawake kuzaa mapacha ni la kibaolojia na halina mahusiano yoyote na mikosi kwa binadamu. 

Daktari wa watoto kutoka hospitali ya Wilaya ya Butimba mkoani Mwanza, Dk Mohammed  Kiwanuka anasema matokeo ya kupata watoto mapacha ni kuwepo kwa vinasaba ndani ya familia au jamii husika ambavyo hurithishwa kizazi na kizazi. 

Pia wanawake wenye umri mkubwa kuanzia miaka 37 wanakuwa na uwezekano wa kupata watoto mapacha. 

Dk Kiwanuka anasema mwanamke kushika mimba ya mapacha lazima awe na mbegu mbili za kiumbe ili mtoto au watoto watengenezwe. 

Kuna mapacha wa aina mbili: aina ya kwanza ni mwanamke anakuwa na yai moja (monozygoty twins) au mayai mawili. Mapacha hawa wa kufanana huzaliwa wakiwa wanavinasaba vinavyofanana.

“Kabla ya hapo mwanamke anakuwa na yai moja linakuja kurutubishwa na mbegu ya mwanaume na baada ya hapo yai linakuja kugawanyika na kuwa watoto wawili,” anasema mtaalam huyo wa afya. 

Aina nyingine ni mwanamke kutoa mayai mawili yaliyopevuka na inapotokea mwanamke akakutana na mbegu ya mwanaume ikarutubishwa basi mapacha wawili wasiofanana wanatokea ambapo mmoja huwa ni wa kike au kiume na wakati mwingine wakawa ni jinsia moja ila vinasaba ni tofauti.

Daktari huyo ameitaka jamii ione hilo ni suala la kawaida la uzazi na lisihusishwe na imani ambazo siyo sahihi.


Soma zaidi:


Nao Viongozi wa dini wameiambia Nukta (www.nukta.co.tz) katika dini zao hakuna ubaguzi wowote kuhusu watoto wanaozaliwa kwa sababu wanaamini watoto ni baraka kutoka kwa Mungu.

Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) Sheikh Khamis Mataka anasema watoto mapacha wanapozaliwa na waumini wa dini hiyo huchukuliwa kama watoto wengine na hulelewa katika misingi yote ya kidini.

“Katika Uislamu suala la mama kuzaa mapacha halina tatizo kwa kuwa hilo ni takwa la mwenyezi Mungu. Dini iliamua kuwaacha watoto wote na kuwapatia baraka zote za kimungu ili waishi na wafurahie uumbaji wa mwenyezi Mungu,” anasema Sheikh Mataka

Anasema dini hiyo inalaani vitendo vyote vya kibaguzi vinavyofanywa na watu kuwabagua watoto kwa sababu haikubaliki mbele za Mungu.

Mtazamo wa Sheikh Mataka unaendana na Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Ziwa Victoria usharika wa Iman Kanisa Kuu, Boniphace Salawa anayesema watoto wakiwemo mapacha hawana shida yoyote ambayo wanaweza kusababisha kwenye familia.

“Tunaamini kwamba watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu ambayo huileta kwa binadamu awe ni mmoja, wawili ama zaidi hiyo tunaamini kuwa ni baraka,” anasema Mchungaji Salawa. 

Mchugaji huyo anasema tangu watoto wanapokuwa wadogo hubatizwa na wala wazazi wao na watoto wenyewe hawapatwi na tatizo lolote katika siku za kuishi kwao. 

Anasema hana ushahidi wa moja kwa moja kwa watoto mapacha kubeba mikosi ya familia kwa sababu familia zao hao watoto ambao amewahi kukutana nazo ziko vizuri tu hazina shida. 

Anaitaka jamii kupuuza maneno ya baadhi ya watu kudai kuwa watoto mapacha ni mkosi na wawatie moyo na kuwalinda wanawake wanaozaa mapacha.

Hata hivyo, Serikali inasema ufanyaji matambiko kwa mapacha ni la kiimani na halina madhara kwa sababu linafanyika kwa uwazi na haliathiri maisha ya mapacha zaidi ya kutimiza mila. 

Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Mwamajila, James Shibiriti anasema jamii ya Wakango wanashirikiana nao vizuri na hata wanapotaka kufanya shughuli zao hufuata taratibu zote ikiwemo kutoa taarifa kwenye ofisi ya kijiji hadi kata ili kujua uwepo wao.

Anasema Serikali haiwachukulii kuwa ni watu wabaya isipokuwa wanaheshimu imani na tamaduni zao wanazozifanya.

Mzee Masomi Shibiriti (aliyekaa) akivalishwa shanga ikiwa ni sehemu ya kukamilisha taratibu ya tambiko la watoto wake mapacha. Picha|Mariam John. 

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Unaweza kusema ni maumivu juu ya maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto vinavyotumia mafuta ya

Unaweza kusema ni maumivu juu ya maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto vinavyotumia mafuta ya

Nukta TV

Neema Mohamed, Mkurugenzi wa Bone and Blood Foundation, ni shujaa wa ugonjwa wa selimundu Sickl

Neema Mohamed, Mkurugenzi wa Bone and Blood Foundation, ni shujaa wa ugonjwa wa selimundu Sickl

Nukta TV

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametua kwenye ardhi ya Urusi kwa ziara ya kitaifa ya siku

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametua kwenye ardhi ya Urusi kwa ziara ya kitaifa ya siku

Nukta TV