Shule 24 vigogo 'zilizoteka' 10 bora kidato cha nne

Daniel Mwingira 0330Hrs   Februari 13, 2018 Habari
  • Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu  Francis na Shule ya Wavulana ya Marian  hazijawi kuwa nje ya 10 bora kitaifa.

  • Shule 11 zimewahi ingia kumi bora katika kipindi cha miaka sita lakini hazijawai rudi tena kumi bora mpaka sasa.

Dar es Salaam. Kila mwaka matokeo ya kidato cha nne yanapotoka mbali na kujua matokeo ya watoto au ndugu zao, wengi hupenda kujua shule 10 vinara nchini. Baadhi hutumia takwimu hizo kufanya maamuzi ya shule za kuwapeleka watoto au ndugu zao. 

Kwa bahati mbaya hivi karibuni imekuwa nadra kuona shule za umma zikiingia kwenye orodha hiyo ya 10 bora katika mtihani wa taifa wa kidato cha nne (CSEE).

Uchambuzi wa matokeo ya CSEE uliofanywa na Nukta Tanzania katika kipindi cha miaka sita ya hivi karibuni umebaini kuwa ni shule 24 tu kati ya zaidi ya  3,039 ambazo zimeonja angalau mara moja nafasi ya shule 10 vinara. 

Katika uchambuzi huo uliofanywa kwa kutumia matokeo ya  shule zenye wanafunzi zaidi ya 40, imebainika kuwa hakuna hata shule moja ya Serikali iliyowahi kufurukuta kuingia kwenye orodha hiyo hivyo kufanya itawaliwe na shule binafsi na mashirika ya kidini.

Kati ya shule hizo zilizofanya vizuri zaidi kwa kipindi hicho nyingi ni zile za wasichana zikiwa 11 kati ya 24 zilizoingia kwenye orodha hiyo. 

Shule za  wavulana zinafuatia kwa kuingia zaidi kwenye orodha hiyo baada ya kuingiza shule saba sawa na theluthi ya shule 24. 

Shule hizo ni Marian Boys ya Pwani), Fedha Boys na Shamsiye Boys za Dar es Salaam, Abbey (Mtwara), Uru Seminari (Kilimanjaro), Don Bosco Seminari(Iringa), Alliance Boys (Mwanza) na Thomas More Machrina. Kundi la mwisho ni shule za  mchanganyiko zinazojumuisha wavulana na wasichana ambazo zipo ni tano. 

Uchambuzi huo unaonyesha Shule ya  Wasichana ya Mtakatifu Francis  na Shule ya Wavulana ya Marian ndiyo shule pekee ambazo hazijawai kuporomoka kutoka katika orodha hiyo ya kumi bora kitaifa.

Mathalani shule ya Wasichana ya Mtakatifu Francis katika miaka hiyo sita imekuwa ya kwanza kitaifa kwa miaka mitatu yaani mwaka 2012, 2013 na mwaka 2017. Miaka mitatu iliyobaki  mwaka 2016  ilikuwa ya pili Kitaifa , mwaka 2015 ilikuwa ya tatu kitaifa na mwaka 2014 ilikuwa ya nne kitaifa.

 Mariani Boys  imewahi kushika nafasi ya pili kitaifa mara mbili mfululizo mwaka 2012 na 2013.Mwaka 2014 ilikuwa ya tatu kitaifa  na mwaka 2015  ilishika nafasi ya sita kitaifa .Mwaka 2016 shule hiyo ilikuwa ya tano na matokeo ya  mwaka 2017 ilikuwa ya tisa kitaifa.

Shule 22 zilizosali ama zimewahi kuingia mara tano na chini ya hapo katika shule kumi bora kitaifa au mpaka mara moja alfu hazikufanikiwa kurudi tena ingawa zinaendelea kufanya vizuri.

Miongoni mwa shule hizo  22 kuna shule tatu ambazo zimefanikiwa kuingia mara tano kati ya sita katika kipindi cha miaka sita.Shule hizo ni shule ya wasichana ya Marian ambayo  mwaka 2015 ilishika nafasi ya kumi na nne kitaifa.

Pamoja na shule ya wasichana ya fedha ambayo ilishika nafasi ya kumi na mmoja mwaka 2016 na  shule ya wavulana ya Fedha mwaka 2013 walikuwa wa 28 kitaifa.

Vile vile shule za  wasichana za Anwarite  na Canossa zote zimefanikiwa kuingia kumi bora mara nne kwa  nyakati tofauti zimekosa mara mbili .Shule ya wasichana ya  Canossa imeshika nafasi ya tano mara tatu kitaifa kuanzia mwaka 2012, 2013 na 2015. Mwaka 2017 imeshika nafasi ya saba kitaifa.

Wakati shule  sita  zimefanikiwa kuingia mara mbili katika kumi bora shule hizo ni  Kaizirege  ambayo imekuwa ya kwanza kitaifa kwa miaka miwili mfululuizo mwaka 2014 na 2015. Sambamba na shule za Abbey Sekondari ya Mtwara (2013-2014), Shamsiye Boys ya Dar es Salaam (2016 na 2017), Bethela Sab Girls (2014 na 2017) na Rosmini sekondari (2012 na 2013) na Alliance Boys.

Na  shule  12 zilizobakia zimefanikiwa kuingia mara moja tu kwenye shule kumi bora kitaifa na hazikuwai kurdi tena  ndani ya miaka sita hiyo ambazo ni Kifungilo girls, Kemebos, St Mary’s Mazinde Juu Secondary School, Precious Blood, Alliance girls , Alliance Rock Amry , St Aloysius Girls , Don Bosco Seminary,Jude Moshono,Uru seminary na Thomas More Machrina.

Matokeo hayo yanatoa tafakari kubwa kuhusu mustakabali wa elimu nchini hususan katika utoaji wa elimu bora katika shule za umma.  Mkakati wa makusudi unahitajika katika kuboresha elimu hasa kwa kuboresha maslahi ya walimu, kuongeza vifaa vya kufundishia pamoja na gharama za utoaji elimu kati ya shule za serikali na binafsi.


Related Post