Zawadi zinazowafaa wanawake sikukuu ya wapendanao

February 14, 2020 10:37 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Baadhi ya zawadi hizo ni za kawaida kabisa ikiwemo viatu, saa za mkononi na peremende.
  • Zawadi kubwa kuliko zote ni kumpa wako akae na wewe.
  • Kama umepanga kumpelekea maua, tafakari upya.

Dar es Salaam. Huenda unapata changamoto kumnunulia mke au mchumba wako zawadi na kila ukitafuta wazo unalikosa. Cha kushangaza ni kwamba, unaweza kujizatiti na kununua zawadi ambayo huenda umpendaye asiifurahie.

Kama wewe ni mmoja kati ya watu wanaopata shida hiyo, hizi ni baadhi ya zawadi ambazo wanawake wengi wanazifurahia. Funga mkanda kisha anza safari hii fupi pamoja nami.

Tembelea duka na nunua peremende mchanganyiko. “Wanawake  wengi hufurahishwa na jitihada ambayo umechukua kujaribu kumfurahisha. Hata kama ukimnunulia pipi kifua kama anakupenda kwa dhati atafurahi,” amesema moja ya wanawake waliofanya mahojiano na Nukta asubuhi ya leo.

Mchukulie msosi. Sidhani kama yupo mwanamke ambaye anaweza asifurahie chakula. Japo siongelei ugali na mlenda, pia siyo mbaya kama unahisi mpenzi wako atafurahi.

Siyo mbaya kama ukimchukulia mpenzi wako kuku choma robo ukampatia atafune tafune wakati ukiwa pembeni yake.

Tembelea duka na nunua peremende mchanganyiko. “Wanawake  wengi hufurahishwa na jitihada ambayo umechukua kujaribu kumfurahisha. Picha|Designthread.

Uliza kiatu kinachomfaa kulingana na mguu wake. Kama yupo mwanadada ambaye hatafurahia zawadi hii nifuate “inbox” kunisahihisha. 

Mwanamuziki anayechipukia Shinuni Masoud, amesema kiatu ni kitu kinachomtambulisha sana mwanamke katika maeneo mbalimbali anayokwenda. 

“Usidharau nguvu ya kiatu. Kusifiwa kiatu ni ndoto ya wasichana wengi,” amesema Shinuni.

Endapo unafahamu shughuli za mpenzi wako, utafahamu kiatu gani kitamfurahisha. Mfano kama mpenzi wako ni mwanasheria, siyo mbaya ukiulizia dukani viatu vinavyovaliwa hasa na wataalam hao.

Kama kiatu ni gharama basi mnunulie marashi na vipodozi. Hii, ni kwa wachache wanaotumia vitu hivi. Kunukia vizuri ni ndoto ya kila mwanamke. Hakuna mwadada ambaye hatajasikia furaha akiambiwa marashi yako ni mazuri.

Hakika hutaki kuikosa nafasi hii ya kumfanya mpenzi wako asumbuliwe na mashosti zake kuuliziwa jina la marashi yake na wapi alipoyapata.

“Chukua muda wako, ulizia kwa wasichana kadhaa kama chaguo lako ni zuri na kisha mnunulie pefyumu mpenzi wako anukie,” amesema mjasiriamali wa vipodozi na vitu vya wanawake Jijini Dar es Salaam, Loyce Msolwa.


Zinazohusiana


Muda! Ndiyo muda ni zawadi kubwa kuliko zawadi zote duniani. Kama umeshindwa kumpa vitu vinavyonekana mpenzi wako, basi muda wako. 

Tumieni muda wenu kwa kutazama filamu, kupika, kutembea tu au kutafakari mambo mbalimbali yanayohusu maisha yenu. 

Kama ilivyo kwa Mwanasheria Faith Robert, kupata muda na mpenzi wake ni kitu cha thamani kuliko.

Kwa zawadi hizo unaweza kumfanya mpenzi wako awe karibu zaidi na wewe na kujiona anapendwa na kuthaminiwa na yule anayemwamini. 

Nilisahu pia zawadi ya maua lakini nilipozungumza na baadhi ya wanawake kuhusu hili, wengi wao  walinicheka na kunijibu “mimi siyo nyuki” na wengine wakisema “siwezi kula maua”.

Ni mada ya siku nyingine lakini wiki ijayo, tukutane kujadili jinsi mwanamke anavyoweza kumsaidia ampendaye afikie ndoto zake.

Enable Notifications OK No thanks