Youtube yaweka vigezo vipya kupata “alama ya uthibitisho”

September 23, 2019 11:13 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Moja ya sifa kubwa anayotakiwa mtu kupata alama hiyo ni  pamoja na kuwa na watazamaji kuanzia 100,000 na kuendelea
  • Alama ya uthibitisho (Verification Badge) inatumiwa zaidi katika kujipatia umaarufu mtandaoni.

Huenda wewe ni mmoja wa watu wanaotamani sana siku moja kuwa na akaunti yenye alama ya uthibitisho (Verification Badge) katika mitandao ya kijamii kama Twitter, Instagram hata Youtube wanaoweka alama hizo kwa watumiaji wake waliokidhi sifa za kupata uthibitisho huo. 

Mtandao wa Youtube ulio chini ya kampuni ya Marekeni ya Google hivi karibuni wameboresha sifa zitakazomlenga mtu mwenye sifa na uwezo wa kupata alama hiyo katika ukurasa wake.

Moja ya sifa kubwa anayotakiwa kuwa nayo mtu ni pamoja na kuwa na watazamaji kuanzia 100,000 na kuendelea, pamoja na utambulisho katika chaneli husika.

Utambulisho unaohitajika ni kama vile kuwa na nembo ya akaunti (Account Logo), lazima iwe inafikiwa na hadhira yoyote na lazima iwe na maelezo yanayoelezea kuhusu akaunti na kuwa na watembeleaji hai (Active users) wanaoifuatilia mara kwa mara. 


Zinazohusiana:


Awali Youtube ilitangaza kufuta alama za uthibitisho katika mtandao huo ili kuweka sifa mpya zinazowataka kupata hizo alama, lakini ilisitisha mpango huo baada ya kuwepo malalamiko kutoka kwa watumiaji wake wakidai kuwa yangewaathiri ikiwemo kuwapotezea umaarufa walioujenga kwa muda mrefu.

Baada ya Youtube kupitia tena maamuzi yake ilifuta  kauli  ya kuziondoa alama hizo kutoka kwenye akaunti za watu waliokuwa nazo hapo awali na kuweka utaratibu mpya.

Utaratibu huo wa sasa unawahusu watu wanaotaka alama hizo za uthibitisho ambazo ni sehemu ya kujipatia umaarufu.

Enable Notifications OK No thanks