Wamarekani waunda kifaa cha kuwasaidia wanaokoroma usingizini

October 23, 2019 2:33 pm · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni kifaa chenye kusaidia mfumo wa upumuaji mtu akiwa kwenye usingizi mzito.
  • Umuhimu wa kifaa hicho kinasaidia mtu kupumua vizuri bila shida pindi anapokuwa kwenye usingizi.

Dar es Salaam. Usingizi ni kitu chenye kuleta afya kwa kila binadamu anaeishi ila namna tunavyolala inatofautiana kulingana na tunavyoweza kuingiza na kutoa pumzi wakati wa kulala. 

Kulala kwa kukoroma kunaweza kusababishwa na ugumu wa kupumua kipindi mtu anapokuwa usingizini au matatizo katika mfumo wa kupumulia katika pua za mtu na kumsababishia kuwa na desturi ya kukoroma pindi anapokuwa kwenye usingizi mzito.

Hali hii huwa kero pale mtu anapokuwa jirani na mwenzie na kusikika akikoroma anapokuwa amelala licha ya kutokujijua kwa sababu anakuwa kwenye usingizi mzito.

Kumalizia tatizo hilo, Wamarekani wamegundua kifaa kinachoitwa Silent Snore kinachosaidia mtu anapokuwa usingizini asisikike kama anakoroma usiku mzima mpaka anapoamka kutoka usingizini.

Kifaa hicho kinafanya kazi kwa kupachikwa kwenye pande zote mbili za pua. Baada ya kukiweka puani kinasaidia mtu kuwa na uwezo mkubwa wa kupumua vizuri bila shida akiwa usingizini hata kama ana desturi ya kukoroma.

Silent Snore inasaidia kupunguza kero ya kukoroma na kuweka mdomo kwenye hali nzuri kwani inasababisha mtu kufumba mdomo pindi anapokuwa amelala kutoana na kifaa hicho kinachowekwa puani.

Kifaa hicho pia kinamweka mtu huru pindi anapokuwa amelala kujua kwamba amelala bila kusumbua watu kwa sauti za kukoroma tofauti na pale anapokuwa hajatumia kifaa hicho usingizini.

Charles Msinde, Daktari katika hospitali ya Mama Ngoma anasema kifaa hicho kinaweza kuwa na umuhimu wa kumsaidia mtu katika ulalaji wake lakini vilevile inaweza kuwa na athari kiafya kwani kinazuia upumuaji unaotakiwa.

“Hakiwezi kuwa effective (fasaha) kwa asilimia 100 kwani ukikibana kwenye pua maana yake kuna mifumo fulani inazuiliwa kutoa hewa pindi mtu anapokuwa usingizini. Hivyo si cha kukizoea sana,” amesema Msinde.

Kifaa hicho kinadaiwa kuwa ni cha kwanza kuletwa kwa ajili ya kuzuia upumuaji mgumu mtu akiwa usingizini na kinatarajia kufika Tanzania karibuni kwa matumizi kwa watu wenye uhitaji na matatizo hayo wakati wa kulala.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV