Vifungashio vinavyokwamisha bidhaa za Tanzania kupenya masoko ya kimataifa

March 3, 2022 1:27 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Baadhi wanashindwa kuwa na nembo ya ubora inayotambulika kimataifa.
  • Gharama za uzalishaji bidhaa za kimataifa watajwa kuwa mtihani.
  • Wafanyabiashara washauriwa kuwa na mipango endelevu ya kuyafikia masoko ya kimataifa.

Dar es Salaam. Uzalishaji wa bidhaa mbalimbali miongoni mwa Watanzania ni mojawapo ya njia inayotumika kupambana na umaskini na ukosefu wa ajira.

Wapo Watanzania wanaojihusisha na uzalishaji wa vitu kama viungo, mafuta, sabuni na usindikaji wa vyakula ikiwa ni sehemu ya wao kujipatia kipato.

Hata Hivyo, kati ya changamoto wanayoipata ni kushindwa kufikia masoko ya kimataifa sababu ikiwa ni kutokukidhi  vigezo vya ubora na ufungashaji wa bidhaa zao.

Mahitaji makubwa kwenye vifungashio kwa bidhaa zinazouzwa kimataifa ni pamoja na kuwa na jina la biashara, msimbo upau (Bar code) pamoja na maelezo ya bidhaa hiyo ikiwemo viungo pamoja na virutubishi kwa ujazo.

Vingine ni matumizi ya lugha ya kimataifa, tarehe ya uzalishaji na kikomo cha matumizi. Nini ambacho kinawakwamisha?

Kinachotofautisha bidhaa yako na bidhaa zingine zote pembeni yako ni kifungashio chako. Picha| Echo Machinery.

Vigezo vya kimataifa ni gharama, kujifungia

Mkurugenzi Mtendaji wa Life Food Enterprises, Christian Phillipo amesema, changamoto wanayopitia wafanyabiashara wengi ni vigezo vya kimataifa vilivyowekwa hasa kwenye masuala ya vyakula.

Phillipo amesema, vigezo vingi vya kupeleka bidhaa kimataifa  vinapimwa kwa viwango vya nchi zilizoendelea na wa Tanzania ambayo ni nchi inayoendelea, inakuwa ngumu kwa wafanyabiashara wake kuvifikia.

Kufikia vigezo hivyo inahitaji teknolojia ya kisasa pamoja na kuwa na mtaji mkubwa kwani utatumia gharama ya juu katika uzalishaji ili kufikia viwango vinavyohitajika kimataifa na kuathiri biashara yako.

“Ukitaka kusafirisha unga wa sembe kimataifa unatakiwa uwe na virutubishi 12 wakati kwa unga wa kuuza hapa hapa unaweka virutubishi vinne tu,” amesema Phillipo akivitaja kuwa ni madini ya chuma, foliki, zinki na vitamini B12.

Jambo lingine alilosema Phillipo ni Watanzania kujifungia nchini badala ya kutembelea nchi zingine ili wenzao wanavyoendesha biashara kimataifa.

“Mfano kwenye hii Dubai Expo, wafanyabiashara wangeenda wangeona teknolojia mpya na kuona namna wanavyoweza kuzitumia katika uzalishaji. Sasa wafanyabiashara wadogo hawaendi, wanaenda wakubwa ambao tayari wana masoko,” amesema Phillipo.


Soma zaidi:


Vifungashio bado bado

Siyo wafanyabiashara wote wa Tanzania wamewekeza kwenye vifungashio vya bidhaa zao.

Ukitembelea maduka makubwa (malls) unaweza kulinganisha ubora wa vifungashio vya bidhaa za nje na za Watanzania. Huenda ukapata jawabu huko. 

Mtaalamu wa biashara wa kimataifa, Safari Fungo ameiambia Nukta Habari (nukta.co.tz) kuwa wafanyabiashara wengi bado wanasumbuka kukidhi mahitaji  ya vifungashio wanavyotumia na hivyo kushindwa kutumia fursa za masoko ya kimataifa.

“Kitu cha kwanza mnunuaji anachokiona shelfu za maduka makubwa ni jinsi bidhaa ilivyofungashwa hivyo ufungashaji na ubunifu unatakiwa uwe kwenye kiwango cha kumwambia mtazamaji anunue,” amesema Fungo.

Mtaalamu huyo wa masoko pia amesema vifungashio vienda sambamba na vibebeo, makreti pamoja na shelfu za maduka ya kimataifa.

Alama za ubora zinazojulikana kimataifa

Baadhi ya wafanyabiashara wanadhani wakishapata cheti cha Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ndiyo wamekamilisha kila kitu lakini mambo sivyo yalivyo.

Mkurugenzi wa kampuni ya kusindika viungo, Get Aroma Spices, Fatma Mbaga amesema kila nchi na vigezo vyake. Mathalani kwa TBS, Mbaga amesema inatambulika kwa nchi za Afrika Mashariki peke yake.

“Kuna bidhaa unaweza kupeleka Marekani zikakubaliwa na bidhaa hizo hizo ukipeleka Japan zinakataliwa,” amesema Mbaga.

Mfanyabiashara huyo anayeuza bidhaa zake katika nchi mbalimbali  amesema kingine kuhusu vifungashio ni matumizi ya plastiki na mifuko katika kupaki bidhaa.

Amesema zipo baadhi ya nchi zilizo na marufuku ya matumizi ya malighafi ya plastiki ikiwemo mifuko. 

Endapo mtu anatumia plastiki kufungia bidhaa yake, ni wazi kuwa soko la nchi hizo atakuwa amelikosa.

Kuna baadhi ya nchi zinapinga matumizi ya plastiki kwenyevifungashio. kuwamakini unapochagua. Picha| Loughborough University

Suluhu iko wapi?

Ili bidhaa za Kitanzania zipenye kwenye masoko ya kimataifa na kushindana na bidhaa za nchi nyingine, yapo mambo ambayo wafanyabiashara wanatakiwa kuzingatia.

Balozi wa vijana kwenye Jumuiya ya Afrika Madhariki (EAC), Jessica Mshama amesema vijana wanatakiwa kuzingatia uwekezaji kwa ajili ya kufikia masoko ya kimataifa.

Mshama amesema watu huanza biashara kwa kuhudumia soko la ndani, na hivyo kupitia ugumu pale wanapotaka kuhamia kwenye soko la kimataifa.

“Wafanyabiashara wawe na mipango wakati wanapoanzisha biashara zao. Kupanua biashara mbeleni itakuwa rahisi kama mpango ulikuwepo tangu mwanzo,” amesema Mshama.

Balozi huyo amesema kuwa na mpango kutamsaidia mtu kuwa na vifungashio sahihi, nembo nzuri ya kibiashara pamoja na kufikia vigezo vya kimataifa mapema. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
7 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
7 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV