Uzalishaji maua, viungo mwendo wa kinyonga

March 29, 2019 10:54 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Bado uzalishaji wa maua na viungo uko chini jambo linalotoa fursa kwa vijana kutumia ardhi iliyopo nchini kuongeza uzalishaji na kufaidika na fursa zilizopo kwenye mazao hayo. 
  • Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki yafungua milango kwa wazalishaji kupata mafunzo Israel. 

Dar es Salaam. Licha ya uzalishaji wa mazao ya matunda kuongezeka, bado uzalishaji wa maua na viungo uko chini jambo linalotoa fursa kwa vijana kutumia ardhi iliyopo nchini kuongeza uzalishaji na kufaidika na fursa zilizopo kwenye mazao hayo. 

Mazao ya bustani yanajumuisha matunda, mboga, maua na viungo vinavyotumika katika shughuli za mapishi. Maua na viungo ni miongoni mwa bidhaa zinazosafirishwa zaidi katika masoko ya nje ya nchi.

Kitabu cha Hali ya Uchumi wa Taifa katika mwaka 2017 kilichotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kinaeleza kuwa mwaka 2017 uzalishaji wa mazao ya bustani uliongezeka kwa asilimia 10.7 ikilinganishwa na asilimia 5.3 iliyorekodiwa mwaka 2016. 

“Hii ilitokana na kuhamasika kwa wakulima kuongeza uzalishaji kufuatia uwepo wa soko la uhakika, kuongezeka kwa usindikaji wa mazao hayo 137 na kuongezeka kwa ulaji wa matunda na mboga,” inasomeka sehemu ya kitabu hicho. 

Hata hivyo, uzalishaji wa maua na viungo uko chini zaidi ukilinganisha na mboga na matunda.

Mathalani katika kipindi hicho wakulima walizalisha tani 11,615 tu za maua ambapo ni chini zaidi mara 451 ya uzalishaji wa matunda ambao ulikuwa tani milioni 5,243,343.

Kutokana na mahitaji ya maua na viungo kuongezeka kimataifa, vijana wanaweza kutumia fursa ya kutumia ardhi iliyopo kuongeza uzalishaji na kupata fursa ya masoko ya nje.


Zinahusiana:


Kutokana na umuhimu wake, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki leo (Machi 29, 2019) imetangaza mafunzo ya vitendo (field attachment) kwenye mashamba makubwa ya mazao mbalimbali yakiwemo ya matunda, mbogamboga, ufugaji, uvuvi na mazao mengine ya biashara kwa ujira maalum nchini Israel

Mafunzo hayo ya miezi 11 kuanzia Septemba, 2019 ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Serikali ya Israel kwa Tanzania ili kuwaongezea ujuzi Watanzania wenye nia ya kuwekeza katika sekta ya kilimo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
21 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
21 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Nukta TV

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

Nukta TV