Usiyoyafahamu kuhusu ujio wa kifaa cha michezo ya kidijitali cha “PS5”

June 15, 2020 12:20 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni teknolojia ya michezo inayotengenezwa na kampuni ya vifaa vya kieleketroniki ya Sony.
  • Inatarajia kuzinduliwa mwishoni mwa mwaka huu.

Dar es Salaam. Bila shaka umesikia minong’ono mingi kwa watu juu ya ujio wa toleo jipya la kifaa cha kielektroniki maarufu kama “Play Station (PS5), lakini bado haufahamu kwa undani suala hilo. 

Kifaa hicho hutumiwa na watu kucheza michezo ya kidijitali ikiwemo mpira wa miguu na mbio za magari kwa kuunganishwa na runinga.

Kifaa hicho cha PS5 kinakuja baada ya toleo la PS4 kukaa sokoni tangu mwaka 2013. 

Kifaa hicho kinachotengenezwa na kampuni ya Sonny kinasubiriwa kwa hamu na wadau hasa kama kitakuja na vipengele vipya kwa ajili ya watumiaji wake.

PS5 inakuja na miundo miwili ambapo moja wapo unaweza kuweka CD. picha| Essentially Sports.

Tunayoyafahamu

Kwa mujibu wa Sony wakati ikifungua pazia la  teknolojia hiyo, PS5 itakuwa sokoni ifikapo msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka 2020. 

Hata hivyo, kwa matoleo mawili ya nyuma ya michezo hiyo, yalitoka mwezi Novemba ambapo manunuzi kwa ajili ya sikukuu huanza na hivyo huenda hata PS5 ikafuata mkondo huo.

Hata hivyo, Sony haijatangaza siku ya uzinduzi wa kifaa hicho.

Bei ya kifaa hicho

Licha ya kwamba Sony haijatangaza bei ya kifaa hicho,  wadau wa michezo ya kidijitali wameanza kutoa makadirio ambayo huenda bei yake ikadondokea hapo.

Kwa mujibu wa tovuti ya Bloomberg gharama za kutengeneza kifaa hicho inakadiriwa ni Sh1.04 milioni ambapo kinaweza kuuzwa kwa Sh1.15 milioni


Zinazohusiana


Kwanini uachane na matoleo ya zamani ya PS ununue PS5?

Kifaa hicho kinakuja na miundo miwili. Moja ni yenye sehemu ya kuwekea diski maarufu kama CD na “PS5 digital edition” ambayo inampa fursa mtumiaji kununua michezo na kuipakua kwenye kifaa chake.

Sony bado haijasema chochote kuhusu utofauti wa vifaa hivyo. Huenda “PS5 digital edition” ikawa na uwezo mkubwa kiutendaji kwa sababu inaruhusu kupakua michezo mtandaoni. 

Jambo hilo huenda likamfurahisha mdau wa michezo hiyo na mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) Prosper Makundi ambaye amesema PS4 ilikuwa inachukua muda mrefu sana kuanza kucheza.

“Waliokuwa na PS4 wameshaanza kuzitafutia wateja wakingoja PS5. Binafsi nategemea iwe na kasi kuliko PS4 kwani inakera kusubiria mchezo usome kwa vijidakika,” amesema Makundi

Utayari wako wa kununua teknolojia hii mwishoni mwa mwaka huu upoje? Endelea kusoma ukurasa huu kwa kufahamu yajayo.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW