Usidanganywe! Apple haigawi simu za iPhone bure

July 11, 2020 8:03 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Kampuni hiyo ya Marekani imezushiwa kuwa inagawa bure simu aina ya iPhone kwa wanafunzi na wafanyakazi.
  • Habari hiyo ni uzushi kwa sababu Apple haijatangaza kutekeleza zoezi hilo wakati huu wa Corona. 

Dar es Salaam. Kama wewe ni miongoni mwa watu ambao wamekutana na taarifa mtandaoni inayosema kuwa kampuni ya Apple inagawa bure simu za iPhone na umeiamini, basi fahamu umedanganywa. Kampuni hiyo haijatoa tangazo kama hilo na ni habari ya uzushi yenye lengo la kupotosha.

Taarifa hiyo inasambaa hasa katika akaunti ya Facebook ya Iphone Giveaway 2020. Ilichapishwa Julai 4, 2020 kwa lugha ya Kiingereza kuwa, “IPHONE LATEST GIVEAWAY FOR STUDENTS AND WORKERS IPHONE company is ready to give away 10,000 brand new phones to people because of this pandemic period.

FREE IPHONE PHONES FOR STUDENTS & WORKERS TO WIN IPHONE Comment a lot of “I” to have a big chance to win!! and to be noticed by us in the comment section No Scammer Please Let’s Help!! ❤️❤️ Then Come inbox! via “SEND MESSAGE” button bellow With the Screenshot of your comment.”

Kwa tafsiri isiyo rasmi taarifa hiyo inaeleza kuwa “iPhone ipo tayari kutoa simu mpya za iPhone 10,000 kwa wanafunzi na wafanyakazi katika kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa wa Corona.

Kupata simu za bure za Iphone kwa wanafunzi na wafanyakazi. unatakiwa kutoa maoni sio utapeli. Tafadhali tusaidiane! Kwa hiyo nitumie maseji ukiambatanisha na picha ya ujumbe wa maoni yako.


Zinazohusiana


Ukweli ni upi?

Habari hizo za ugawaji wa simu za Iphone ni za uongo kwa kuwa Apple haijatangaza popote kuwa inaendesha zoezi hilo. 

Nukta Fakti imepitia  tovuti za kampuni ya Apple Inc sambamba na mitandao yake yote ya kijamii  inayomiliki, hakuna taarifa zozote za ugawaji wa simu hizo za Iphone.

Pia Apple haina uhusiano wowote na akaunti ya Iphone Giveaway 2020 ambayo ilifunguliwa Julai 4 na kuchapisha taarifa hiyo ya ugawaji wa simu hizo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
24 Oct, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
25 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Namna uhaba wa nyani, pofu unavyohatarisha ndoa za Wahadzabe

Namna uhaba wa nyani, pofu unavyohatarisha ndoa za Wahadzabe

Nukta TV

Hii ndio mikoa yenye watu wenye kipato kikubwa zaidi Tanzania

Hii ndio mikoa yenye watu wenye kipato kikubwa zaidi Tanzania

Nukta TV

Uhaba wa maji unavyozitesa jamii za asili, wakiwemo Wahadzabe, Karatu, Tanzania

Uhaba wa maji unavyozitesa jamii za asili, wakiwemo Wahadzabe, Karatu, Tanzania

Nukta TV