Ushirikiano kati ya vyuo, sekta binafsi kuwapika upya wahitimu elimu ya juu

February 9, 2026 6:28 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja na na taasisi binafsi kushirikiana na vyuo vya elimu na kutoa ufadhili kwa wanafunzi wa fani mbalimbali 

Dar es Salaam. Makamu wa Rais, Balozi Dk Emmanuel Nchimbi, amezitaka taasisi binafsi kushirikiana na vyuo vya elimu kuwapika upya wahitimu wa elimu ya  juu kupitia mpango mpya wa kuunganisha sekta hiyo na taasisi za elimu za juu.

Balozi Nchimbi aliyekuwa akizungumza leo Februari 9, 2026 wakati wa uzinduzi wa mpango wa ushirikiano kati ya vyuo na viwanda, ameeleza kuwa sekta binafsi inaweza kuchangia maendeleo ya elimu kupitia mpango huo.

“Kwa kufadhili tafiti na kutoa ufadhili kwa wanafunzi wa fani mbalimbali kulingana na mahitaji ya soko la ajira,” amesema Dk Nchimbi, akisisitiza kuwa hatua hii ni muhimu katika kuhakikisha utekelezaji wa mpango huo unafanikishwa.

Mpango wa pamoja wa ushirikiano katika vyuo na viwanda ni miongoni mwa juhudi za Serikali rasmi kuunganisha vyuo vikuu na masoko ya ajira nchini hususani katika sekta binafsi.

Kupitia mpango huo wanafunzi wa elimu za juu nchini watapata ujuzi unaokidhi mahitaji ya soko la ajira katika sekta mbalimbali nchini suala litakalooongeza rasimali watu na kupunguza changamoto za ukosefu wa ajira nchini.

Ili mpango huo uweze kuleta matokeo chanya Dk Nchimbi amehimiza utekelezaji wa vitendo wa mpango huo ukiwashirikisha waajiri na wamiliki wa viwanda katika katika hatua mbalimbali ikiwemo uandaaji wa mtaala, ufundishaji, kufanya tathmini na kuimarisha miundombinu ya mafunzo.

Awali, Dennis Londo, Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara akizungumza katika hafla hiyo amesema kuwa mpango huu ni nyenzo muhimu ya kufanikisha ukuaji wa uchumi wa Taifa.

Londo amesema kuwa bado kuna pengo kati ya ujuzi unaotolewa na taasisi za elimu na mahitaji halisi ya sekta ya uzalishaji, na amesisitiza umuhimu wa mpango huo katika kuimarisha mitaala na kuongeza mafunzo kwa vitendo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...

Enable Notifications OK No thanks