Unatafuta filamu ya wikiendi? Confidential Spenser inakusubiri

May 29, 2020 3:11 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni filamu inayohusu ushirikiano kati ya vyombo vya dola na nguli wa madawa ya kulevya.
  • M’baku, Spenser na Bokeem Woodbine wote kwenye filamu moja.
  • Vipigo vya paka mla mboga, ucheshi na simanzi, ni vitu utakavyokutana nayo kwenye filamu hiyo.  

Dar es Salaam. “Ni lazima tuufumue huu ukweli. Upo pamoja na mimi?” ni swali la Spenser akimuuliza Hawk.

Safari ya wawili hao inaanza baada ya Spenser kutoka gerezani na usiku huo huo, polisi asiyempenda anatembelewa na malaika mtoa roho.

Wakati anadhani mashtaka yatarudi kwake, Pap! Kesi inaangukia kwa Terrence ambaye ni kati ya mapolisi safi aliowafahamu Spenser.

Shughuli inaanza kufuatilia haki ya Terrence ambaye pia, anakutwa nje ya nyumba yake bila uhai. Hivyo, mkeka uliosukwa na mapolisi unakuwa umekamilika.

Terrence azikwe kama muuwaji akiacha mkewe na mtoto na Captain Boylan, mkuu anayekalia ushahidi na kukandamizia wasio na hatia, azikwe kwa heshima zote za kipolisi.

Umezowea bunduki? Hii ni filamu iliyojaa maadui wanaojua kutumia mapanga na visu dhidi ya anayejiita “Stelingi”.


Zinazohusiana


Kipigo cha paka aliyedokoa mboga, ndicho anachoambulia Spenser ambaye amejitosa kuutafuta ukweli uliojificha nyuma ya pazia la vifo vya maaskari hao wawili.

Patashika nguo kuchanika inayotokea ikikuacha na vicheko vya hapa na pale, inapatikana kwenye kisa cha filamu ya “Spenser Confidential” inayoelezea jinsi vyombo vya dola vina mkono mrefu kupambana na maovu yanayoendelea kwenye jamii.

Unataka kufahamu zaidi? Pakua na lipia kifurushi chako kwenye programu tumishi ya Netflix kufurahia utamu huo utakaokufungia wikiendi yako ya mwisho wa mwezi Mei.

Bando lako tu la intaneti litakutosha kuona nyota walioshiriki kwenye filamu kabambe zikiwemo za “Black Panther” na “Daddy’s Home” kwenye filamu moja. 

Ulimfurahia M’baku kwenye Black panther? Hatokuangusha kwenye filamu hii.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV