UN kuingilia kati sakata la kukamatwa Mwanzilishi wa WikiLeaks

April 12, 2019 10:07 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Muasisi wa mtandao wa WikiLeaks Julian Assange. Picha!Mtandao.


  • Imesema inatathmini kama kukamatwa kwa Muasisi wa mtandao huo Julian Assange na polisi wa London katika ubalizi wa Ecuador nchini Uingereza kulikiuka haki yake ya faragha. 
  • WikiLeaks anashtumiwa na nchi mbalimbali ikiwemo Marekani kwa kuvujisha siri za taasisi zake. 

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa (UN) kuhusu haki ya faragha, Joe Cannataci amesema anatathmini kama kukamatwa kwa Muasisi wa mtandao wa WikiLeaks Julian Assange na polisi wa London katika ubalizi wa Ecuador nchini Uingereza kulikiuka haki yake ya faragha. 

Assange alikamatwa na polisi jana (Aprili 11, 2019) baada ya kukaa katika ubalozi huo kwa takriban miaka saba akikwepa kukamatwa na polisi kwa madai ya kushiriki katika vitendo vya ukatili wa kingono na ubakaji nchini Sweden na ushiriki wake katika kufichua siri za mawasiliano za taasisi za Marekani. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na UN inaeleza kuwa Cannataci anaiandikia serikali ya Uingereza kuomba ruhusa ya kumtembelea Assange Aprili 25, 2019 ili kufanya naye mazungumzo kuhusu hofu ya kukiukwa kwa haki yake ya faragha na kusafirishwa hadi Marekani kwa ajili ya kushtakiwa. 

“Natumai kukutana naye akiwa mtu huru na endapo atakuwa amesafirishwa kupelekwa Marekani kama ambavyo Assange amekuwa akileza hofu yake hadharani kwamba hilo ndilo litatokea, nitaomba fursa moja kwa moja kwa serikali ya Marekani na  popote atakapokuwa ameshikiliwa au kupelekwa wajibu wangu utamfuata,” amesema Cannataci katika taarifa hiyo iliyotolewa jana baada ya Assange kukamatwa.

Amebainisha kuwa  wajibu wa mtaalam maalum wa UN kuhusu haki ya faragha katika kesi ya Assange utaendelea bila kuingiliwa hadi pale watakapokuwa katika nafasi ya kutoa ripoti ya tathimini yao.

Vyombo vya habari vya kimataifa vinaeleza kuwa Assange alitimuliwa katika ubalozi wa Ecuador baada ya Taifa hilo la Amerika Kusini, kuamua kufuta kibali cha uhamiaji kutokana na sababu za kisiasa ambacho kilimpa Assange ulinzi wa kutokamatwa kwa kipindi cha karibu miaka saba.


Soma zaidi:


Kwa mujibu wa UN, Assange ni raia wa Australia ambaye ni mtaalam wa programu za kompyuta ambapo mwaka 2006 alizindua mtandao wa Wikileaks. 

Alipata umaarufu zaidi  mwaka 2010 baada ya kuvujisha kashfa za vita vya Afghanistan na vita vya Iraq.

Kufuatia kashfa hizo serikali ya Marekani ilianzisha uchunguzi wa makosa ya jinai dhidi ya WikiLeaks na kuomba msada kwa mataifa washirika kumkamata Assange..

Baadaye mwaka 2010, Sweden ilitoa kibali cha kimataifa cha kumkamata Assange ambaye miezi mitatu kabla ya hapo alihojiwa kwa madai ya ukatili wa kingono na ubakaji, madai ambayo Assange aliyakana na kusema atasafirishwa kwenda Marekani kwa sababu ya ushiriki wake katika kuchapisha nyaraka za siri za nchi hiyo.

Taarifa ya UN inaeleza zaidi kuwa Disemba 7, 2010 Assange alijisalimisha kwa polisi wa Uingereza lakini aliachiwa kwa dhamana  kwa sababu ya kutofanikiwa kupinga kusafirishwa kwenda Marekani,  

Assange alipewa hifadhi na Ecuador Agosti 2012 na aliishi kwenye ubalozi wa Ecuador nchni Uingereza mpaka Aprili 11, mwaka 2019 alipokamatwa. 

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...