“The Old Guard”: Jeshi la watu watano dhidi ya dunia
- Ni filamu inayohusu mashujaa walio na uwezo wa kupona majeraha yoyote.
- Wanapoibuka watu wanaohitaji vinasaba (DNA) vyao wanajikuta katika mtego wa kumaliza maisha yao.
- Katika filamu hiyo utashudia mapambano yasiyo na kifani.
Dar es Salaam. Kundi la watu wanne ambao ni mashujaa wanajikuta katika hatari baada watu kuanza kuwafuatilia ili kuchambua vinasaba vyao.
Ni baada ya watu hao kufahamu kuwa mashujaa hao wana nguvu ya kupona majereha yoyote wanayopata na hivyo kuwa na uwezo wa kutokufariki dunia.
Nani asiyetaka kuishi milele? Tena bila maumivu ya muda mrefu?
Baada ya wanne hao wakiongozwa na Andy (Charlize Theron) kufahamu kuwa ni panya wanaosubiriwa kunasa kwenye mtego wa paka, wanaanza kupigania maisha yao.
Loo! Kumbe yupo mwingine mwenye nguvukama wao na hawamfahamu. Baada ya kumfahamu, inabidi wamlinde kwa kuwa hafahamu ni nini kipo ndani yake.
“Tumeilinda dunia hii tukipigana katika vivuli. Ni kama haiwezekani kabisa kutoweka katika dunia tunayoishi kwa sasa,” anasema Andy akimwambia binti Nile Freeman (Kiki Layne).
“Wanaenda kutufungia na kutujaza na silaha. Lakini hawajawahi kukutana na jeshi kama letu” Andy anamsisitizia Freeman.
Zinazohusiana
- “Da 5 Bloods”: Filamu itakayokufundisha maana halisi ya uzalendo
- Jifunze nguvu ya familia katika filamu ya “Coffee and Kareem”
- Hapa ndipo uhalifu unapowaunganisha wapendanao
“Jeshi la watu wa tano? Hebu tuanzishe bendi,” anatania Freeman.
Kama umezoea kuwaona wanawake kujipamba kwa mapambo na kufurahia maisha, unahitaji kubadilisha mtazamo wako kwa kumtazama Andy ndani ya filamu ya “The Old Guard”.
Humo yupo na Booker (Matthias Schoenaerts), Joe (Marwan Kenzari), na Nicky (Luca Marinelli) huku wakiwindwa na kiongozi Copley (Chiwetel Ejiofor).
Watakamatika? Nguvu zao zitawasaidia? Na Freeman, ataweza kuendana na kasi ya wenzie?
Shuhudia mapanga, risasi na silaha zisizo na majina kwa kutazama filamu hii kwenye Neftlix ifikapo Julai 10.
Latest
