Tanzania kuzalisha ajira milioni 6.5 sekta ya viwanda
June 30, 2025 5:34 pm ·
Mwandishi
- Kati ya ajira hizo, milioni 1.04 ni za moja kwa moja.
- Ajira hizo zitatoka kwenye viwanda 9,045 vitakavyojengwa.
Dar es Salaam. Waziri wa Viwanda na Biashara Dk Sulemani Jafo amesema Serikali inakusudia kujenda viwanda 9,045 vitavyozalisha ajira milioni 6.5, jambo litakalosaidia kuboresha maisha ya Watanzania na kuinua uchumi wa nchi.
Dk Jafo aliyekuwa akizungumza katika ufunguzi kaulimbiu mpya ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) mmoani Morogoro leo Juni 30, 2026 amesema kati ya ajira hizo zitakazozalishwa, milioni 1.04 ni za moja kwa moja ambazo zina mchango wa moja kwa moja na maisha ya Watanzania.
Aidha, Waziri amewataka maafisa biashara kusimamia mfumo wa stakabadhi ghalani ili kuwasaidia wakulima kupata bei stahiki za mazao yao.
Latest
2 days ago
·
Goodluck Gustaph
Idadi ya watu Zanzibar kuongezeka hadi milioni 2.16 mwaka 2026
3 days ago
·
Kelvin Makwinya
Smartphone 5 zilizopendwa zaidi 2025
3 days ago
·
Kelvin Makwinya
Fahamu wanamichezo 10 wanaolipwa zaidi duniani 2025
3 days ago
·
Kelvin Makwinya
Uhamiaji yatangaza nafasi za ajira kwa vijana Tanzania