Soda au bia: Bidhaa gani huchangia zaidi kwenye mapato?

February 4, 2019 3:16 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Dar es Salaam. Kila tukinunua sehemu kubwa ya bidhaa au huduma kuna asilimia 18 ya bei tunayolipa hukatwa kama Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa mujibu wa sheria.

Hata hivyo, uliwahi kujiuliza ni bidhaa gani Tanzania Bara huchangia kwa kiwango kikubwa mapato katika kipengele hicho cha kodi?

Ripoti ya takwimu za kodi ya mwaka 2016/17 iliyochapishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inaonyesha bia ndiyo bidhaa inayochangia kwa kiwango kikubwa mapato ya VAT ikilinganishwa na bidhaa nyingine. Mapato ya kodi ni muhimu katika utoaji wa huduma za kijamii kama afya, elimu na ujenzi wa miradi ya maendeleo zikiwemo barabara.

Katika mwaka wa fedha wa 2016/17, bia zilichangia asilimia 30 ya mapato yote ya aina hiyo ya kodi. Hii ina maana kuwa Sh100 iliyokusanywa kwenye VAT, Sh30 ilichangiwa na bia. 

Mchango huo wa bia kwenye mapato ya kodi ya VAT ni zaidi ya mara tatu na nusu ya yale yaliyokusanywa kutoka kwenye vinywaji baridi kama soda na juisi.

Fuatilia grafu hiyo kwa habari zaidi juu ya mchango wa bidhaa za ndani katika mapato nchini.

 

Made with Flourish
Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
26 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
27 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
27 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Nukta TV