Simu za mkononi kinara matumizi ya vifaa vya kielektroniki majumbani
- Matumizi ya simu katika kaya yamefikia asilimia 78.1 hadi mwaka 2017 ikiwa ni mara tatu zaidi ya matumizi ya televisheni.
- Mabaki ya vifaa vya umeme na kielektroniki huchangia uharibifu wa mazingira.
Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Ripotiya Takwimu za Taifa za Taka za Kielektroniki ya mwaka 2019 iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inaeleza kuwa simu za mkononi ndiyo zinaongoza kwa matumizi makubwa ya vifaa vya umeme na kielektroniki vinavyotumiwa na kaya za Tanzania Bara.
Ripoti hiyo inaeleza kuwa matumizi ya simu katika kaya yamefikia asilimia 78.1 hadi mwaka 2017 ikiwa ni mara tatu zaidi ya matumizi ya televisheni ambazo hutumika kupata taarifa mbalimbali ili kuwawezesha watu kufanya maamuzi katika shughuli za maendeleo.
Hata hivyo, mabaki ya vifaa vya umeme na kielektroniki huchangia uharibifu wa mazingira huku ripoti hiyo ikieleza kuwa uanzishwaji wa sera na sheria maalum zinazosimamia taka za kielektroniki unaweza kusaidia udhibiti wa taka hizo na kuokoa mazingira.