Serikali yakanusha madai ya Rio kusafisha taswira ya Tanzania kisiasa

May 23, 2026 1:47 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Ufuatiliaji wa Nukta Fakti umebainisha kuwa chapisho linalosambaa halijachapishwa na Habari Maelezo na halipo kwenye kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya chombo hicho cha habari.

Dar es Salaam. Hivi karibuni kuna chapisho ambalo limesambaa kwenye mitandao ya kijamii likidai kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa  na Michezo, Paul Makonda amesema amemleta nahodha wa zamani wa klabu ya Manchester United, Rio Ferdinand kwa lengo la kusafisha taswira ya Tanzania baada ya matukio ya vurugu za Oktoba 29.

Chapisho hilo limechapishwa Mei 22, 2026 kupitia mtandao wa instagram na ukurasa unaojulikana kwa jina la thedartimes likiwa na mfanano wa machapisho ya chombo cha habari cha Serikali cha Habari Maelezo.

“Mauaji yaliyotokea Oktoba 29 yameiachia doa kubwa sana nchi yetu kimataifa. Rio Ferdinand amekubali kutusaidia kuitangaza Tanzania tena duniani ili Nchi yetu iwe safi na watalii waje kwa wingi zaidi. Tukitaka uchumi wetu uendelee kuwa juu, tunawahitaji watu kama Rio Ferdinand” linasomeka chapisho hilo.

Ukweli ni huu

Uchunguzi wa Nukta Fakti imejirishisha kuwa chapisho hilo si halisi na maneno yaliyoandikwa kwenye chapisho hilo hayajasemwa na Waziri Makonda.

Ufuatiliaji wa Nukta Fakti umebainisha kuwa chapisho linalosambaa halijachapishwa na Habari Maelezo na halipo kwenye kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya chombo hicho cha habari.

Aidha, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amethibitisha jana Mei 22, 2026 kwa kuchapisha kwenye mitandao yake ya kijamii kuwa chapisho hilo si halali na ujumbe uliobebwa kwenye chapisho hilo haujasemwa na Makonda.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
30 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
30 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
30 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Vodacom Tanzania yapendekeza gawio la Sh23.91 kwa hisa 2026

Vodacom Tanzania yapendekeza gawio la Sh23.91 kwa hisa 2026

Nukta TV

Fursa kwa wakulima, uhitaji mazao ya chakula ukiongezeka Kenya, Uganda

Fursa kwa wakulima, uhitaji mazao ya chakula ukiongezeka Kenya, Uganda

Nukta TV

Jinsi afya ya akili inavyowatesa wanawake makazini

Jinsi afya ya akili inavyowatesa wanawake makazini

Nukta TV