Serikali kuweka mazingira rafiki mbio za marathon Tanzania

October 25, 2021 11:31 am · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link

Naibu Waziri wa MaliasiLi na Utalii, Marry Masanja akizungumza na watoto wenye ulemavu walioshiriki mbio za marathon za kilomita tano. Picha |Mariam John.


  • Itaandaa vijana wenye vipaji watakaoshiriki mashindano ya kimataifa.
  • itazitumia mbio hizo kutangaza vivutio vya utalii.

Mwanza. Serikali imesema itaendelea kuweka mazingira rafiki katika michezo yote hususani riadha ili kuandaa vijana wengi wenye vipaji watakaoshiriki mashindano hayo na kutangaza vivutio vya utalii kimataifa.

Naibu Waziri wa Utalii, Marry Masanja, akizungumza katika kilele cha mbio za Rock City Marathon ambazo zimefanyika jijini Mwanza Oktoba 24 na kushirikisha zaidi ya wakimbiaji 1,000, amesema pamoja na mbio hizo kuimarisha afya ya mwili lakini pia zinasaidia katika kuhamasisha utalii.

“Michezo ni fursa na fursa lazima tuitumie kuandaa vijana watakaowakilisha Taifa kwenye mashindano ya kimataifa, lakini pia itahamasisha kutangaza utalii, na kama serikali tutahakikisha tunaweka nguvu kwenye msimu ujao ili uwe wa kipekee,” amesema Masanja.

Katika mbio za kilomita 5, 10 na 21, Naibu Waziri huyo alitoa ofa kwa washindi kuanzia wa kwanza hadi tatu wa mbio zote kwenda kutalii kwenye kisiwa cha Saanane.

Wakati mashindano hayo yakikikamilika, Mtanzania Alphonce Simbu alishinda mbio za kilomita 21 kwa wanaume huku kwa upande wa wanawake mbio za urefu huo zilichukuliwa na Cheruta Ester kutoka Kenya.

Emmanuel Mzava ni meneja wa benki ya biashara ya Kenya (KCB) mkoani Mwanza anasema wameamua kudhamini mbio hizo ili kukuza ajira.

“Tunaunga mkono Serikali katika suala la ajira , unapotoa ajira kwa vijana unatoa suluhisho kwenye jamii, na sisi kama KCB tumeona ipo haja kudhamini mashindano hayo ili washindi wanapopata zawadi wanakuwa wamewasaidia kwa namna moja ama nyingine kwenye suala la ajira,” amesema Mzava.

Meneja huyo wa tawi la KCB Nyanza amesema katika mashindano hayo walikuwa wamedhamini zaidi ya wakimbiaji 500 waliokimbia mbio za kilomita 10.

Waliangalia kundi hili kwa kwa sababu ni kundi la kati na linaweza kukimbiwa na watu wengi wakiwemo vijana na watu wenye familia.

Anasema huu ni msimu wao wa pili kudhamini mbiyo hizo na kuwa matarajio yao ni kuja kuwa wadhamini wa kuu.

“Riadha inasaidia kutangaza utalii, hivyo tumeona ipo haja ya kusaidiana na Serikali katika kuwasaidia vijana na wafanyabaishara katika kukuza uchumi wa nchi,” amesema  Mzava.

Rais wa chama cha riadha nchini, Silas Lukas amesema mbio hizi ni za 22 toka zianzishwe na kuwa kadiri miaka inavyoenda ndivyo zinazidi kukua na kuimarisha uchumi wa nchi.

Anasema washiriki wanatoka maeneo tofauti ndani na nje ya nchi na kuwa baada ya mbio hizo baadhi ya washiriki hutembelea hifadhi za Taifa za Rubondo, Saanane na Burigi Chato.

“Hata sasa ninazo taarifa za washiriki ambao baada ya mbio hizi wataenda kutembelea mbuga ya wanyama Burigi Chato,” amesema Lukas.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
14 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV