Sababu ya vyoo vya kisasa kuwa na vitufe viwili vya “kuflashi” maji

January 3, 2020 11:27 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni vile vinavyotumika kuondoa uchafu baada ya haja ndogo na kubwa.
  • Vitufye hivyo vinasaidia kuwa na matumizi mazuri ya maji kwani maji yanatumika kwa kiasi kinachotakiwa kulingana na uhitaji.
  • Vinasaidia kuokoa matumizi makubwa ya maji na ni mbadala pale kimoja kinapoacha kufanya kazi.

Dar es Salaam. Kama wewe ni mtumiaji wa vyoo vya kisasa vya kuflashi hasa vile vya kukaa, basi vitufe vya kusukuma maji baada ya kumaliza haja siyo vigeni kwako. 

Lakini umewahi kujiuliza kwanini kuna vitufe viwili (button) na siyo kimoja? Nini hasa kazi yake? Majibu yote ya maswali yako ambayo huenda umekuwa ukijiuliza bila kupata majibu, leo utayapa katika uchumbuzi uliofanywa na www.nukta.co.tz wa kazi za vitufe hivyo viwili ambavyo ni muhimu kwa watumiaji wa vyoo.

Kimsingi, vitufye hivyo ambavyo vyote viko sehemu moja lakini vinatofautiana ukubwa vinafanya kazi moja tu ya kumwaga maji ili kuondoa uchafu baada ya mtu kujisaidia na kuyaweka mazingira ya choo katika hali ya usafi.

Vinaokoa shida ya matumizi makubwa ya maji kulingana na uhitaji. Picha | Mtandao.

Lakini matumizi yake ni zaidi ya hapo. Tovuti ya Entertainment Times, inaeleza kwa undani umuhimu wa vitufe kuwepo kwenye choo. 

Kitufe kikubwa kipo kwa ajili ya kuflashi maji kuanzia lita sita hadi lita tisa ambayo yanaweza kutumika kusafisha haja ngumu (Solid waste) iliyopo katika choo na kusafishika kwa urahisi zaidi. 

Kile kidogo kina uwezo wa kusukuma lita tatu hadi lita 4.5 za maji na hutumika zaidi kuondoa uchafu ulio katika hali ya maji maji ukiwemo mkojo.


Zinazohusiana:


Faida zake kwa watumiaji

Vitufye hivyo vinasaidia kuwa na matumizi mazuri ya maji kwani maji yanatumika kwa kiasi kinachotakiwa kulingana na uhitaji uliopo kwa muda maalum kwa mtumiaji.

Mathalani, mtu ambaye amepata haja ndogo yaani mkojo atatumia kitufe kidogo na siyo kikubwa ili kuepuka kutumia maji mengi bila sababu za msingi. 

Pia vinasaidia kuwa na mbadala pale kimoja kinapoacha kufanya kazi kwa sababu mtu ana uwezo wa kutumia kingine tofauti na vyoo vyenye mfumo mmoja wa kuflashi ambapo ukipata hitilafu mfumo mzima wa usambazaji wa maji unasimama. 

Vitufe hivyo husaidia kuokoa kiasi kikubwa cha fedha kinachoelekezwa katika kulipia bili za maji, tofauti na vyoo vyenye mfumo mmoja wa maji ambao unaweza kuwa unatumia maji mengi na kupotea bure. 

Licha ya kuwa vitufe vina maana kubwa katika matumizi ya choo, bado usahihi wa utumiaji wake hutegemea zaidi utashi na uelewa wa watu juu matumizi bora ya choo ili kulinda afya. 

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW