Zifahamu faida za kula wadudu lishe

February 9, 2023 1:34 pm · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Takribani asilimia 80 ya mwili wa mdudu umeumbwa na protini na virutubisho, ambapo protini yake inazidi ile ya mnyama afugwaye.

Dar es Salaam. mewahi kufikiria kuwa wadudu ni moja ya majawabu ya kukabiliana na madhara ya mabadiliko ya tabianchi, lishe na kutokomeza umaskini? 

Kama hapana, basi Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo Duniani, (IFAD) unaeleza kuwa wadudu ni chakula muhimu kwa afya ya binadamu na utunzaji wa mazingira. 

IFAD inasema wadudu ni chanzo bora za protini na madini mwilini. Uzalishaji wake unaweza kufanyika bila kutoa kiwango kikubwa cha hewa chafuzi kwa mazingira.

Wadudu ni chanzo muhimu cha chakula kwa takribani watu bilioni 2 duniani, lakini katika nchi za magharibi ni zama hizi ambapo mataifa hayo yameanza kutathmini nafasi ya wadudu katika mifumo yao ya chakula.

Kwa kuzingatia gharama ndogo ya uzalishaji na nafasi ndogo inayohitajika, hata kwa watu maskini wanaweza kukusanya, kufuga, kuchakata, kuuza na kula wadudu.

“kukiwa na zaidi ya aina 2,000 za wadudu wanaoweza kuliwa na binadamu na wanyama, kuanzia nyenje, washawasha, hadi senene—kuna aina nyingi sana ya wadudu watamu ambao tunaweza kuchagua,” inaeleza IFAD.

Faida za kula wadudu

IFAD inaeleza kuwa mtu akijenga mazoea ya kula wadudu atapata faida hizi:

  • Takribani asilimia 80 ya mwili wa mdudu umeumbwa na protini na virutubisho, ambapo protini yake inazidi ile ya mnyama afugwaye.
  • Wadudu wana kiwango kidogo cha mafuta, wanga na wamesheheni vitamini, madini na kamba kamba (fibres).
  • Minyoo nayo ina kiwango sawa cha Omega-3 kama kwenye samaki.
  • Wadudu hawaambukizi magonjwa kwa binadamu na wanyama kama ilivyo kwa wanyama.

Enable Notifications OK No thanks