Programu hii inavyopambana na habari za uzushi kuhusu Corona
December 3, 2020 6:53 am ·
Rodgers Raphael
Dar es Salaam. Mara nyingi pale matukio kama mlipuko wa ugonjwa wa Corona yanapotokea, ndipo picha zinazohusiana na matukio hayo zinapoanza kusambaa kwa kasi kupitia mitandao ya kijamii huku zikisababisha taharuki na hofu kwa watu wanaofikiwa nazo.
Mfano wa picha hizo ni matukio ya mwisho wa dunia, watu kufa kikatili katika mitaa mbalimbali, milipuko ya majengo na nyingine ambazo huenda zikakupatia taharuki itakayokuachia maumivu.
Hata hivyo, wakati mwingine picha hizo huwa siyo za kweli na haziendani na tukio lililotokea kwa wakati huo kwani baadhi huwa ni picha kutoka kwenye filamu, zingine zikiwa ni picha zilizotengenezwa kwa malengo fulani.
Utawezaje kung’amua picha hizo? Simu yako ya mkononi tu inakutosha. Tazama video hii kujifunza.
Latest

13 hours ago
·
Kelvin Makwinya
Wizara ya Katiba na Sheria yaomba Sh687 bilioni kutekeleza vipaumbele 22

1 day ago
·
Kelvin Makwinya
INEC yasisitiza kuzingatia sheria, maadili uandikishaji daftari la kudumu la wapiga kura

2 days ago
·
Kelvin Makwinya
Jinsi ya kupunguza matumizi ya intaneti kwenye simu yako

2 days ago
·
Kelvin Makwinya
Viwango vya kubadili fedha Aprili 29, 2025