Rais Samia awataka wananchi Mwanza kujiandikisha daftari la wapiga kura Serikali za Mitaa 2024 

October 12, 2024 3:18 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Asema idadi ya waliojiandikishakupiga kura jijini humo ni ndogo.

Arusha. Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa jiji la Mwanza kushiriki katika zoezi la kujiandikisha katika daftari la kupiga kura la Serikali za Mitaa linaloendelea kufanyika nchini.

Rais Samia aliyekuwa akizungumza na na wananchi wa Pasiansi Jijini Mwanza leo Oktoba 12, 2024 baada ya kuwasili jijini humo kwa ajili ya kuhitimisha mbio za mwenge na wiki ya vijana ambapo amesema idadi ya waliojiandikisha jijini humo ni ndogo hivyo wajitokeze ili kukamilisha zoezi hilo.

“Ili mambo yaendelee kuwa mazuri hivi twendeni tukajiandikishe katika maeneo yetu na ile tarehe ikifika 27 itakuwa siku ya jumatano na nilisema jana nitaitangaza kuwa siku hamna kazi ili watu wote kazi yetu iwe kupiga kura…

…Mwanza mkitoka hapa nendeni mkajiandikishe ni dakika chache tu unaandikwa unaodoka zako,”amesema Rais Samia.

Wito wa Rais Samia unakuja wakati ikiwa leo ni siku ya pili tangu zoezi la kujiandikisha katika daftari la kupiga kura la Serikali za Mitaa kwa mwaka 2024 nchini lianze huku likitarajiwa kumalizika Oktoba 20 mwaka huu.

Mara baada ya zoezi la kujiandikisha, litafuata zoezi la kampeni kwa siku saba na kisha uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27 mwaka huu zoezi linalotarajiwa kufanyika kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa 10 jioni.

Mbali na kuhitimisha kilele mbio za mwenge ambazo zinatimiza miaka 60 tangu kuanzishwa kwake na wiki ya vijana kitaifa Rais Samia leo atakutana na viongozi wa dini wa mkoa wa Mwanza pamoja na kufunga maonesho ya  teknolojia na uwezeshaji katika sekta ya madini mkoani Geita siku ya kesho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Enable Notifications OK No thanks