Project Power: Filamu mpya ya Netflix itakayoingia sokoni Agosti 14

July 24, 2020 8:13 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni filamu inayohusu kampuni inayotengeneza vidonge vya kuwapatia watumiaji wake nguvu za dakika tano.
  • Art na wenzake wanaungana kupambana na kampuni hiyo ambayo vidonge vyake vinawapatia watu nguvu ya kufanya uhalifu.
  • Wewe ungefanyaje iwapo leo utapewa kidonge cha kukufanya usionekane kwa dakika tano?

Dar es Salaam. Kama wewe umewahi kutazama filamu za kufikirika ulipokuwa mdogo, basi kuna filamu ambazo zilikupatia msisimko fulani na huenda zilikupa hisia za kujiona una nguvu ya ajabu kama walizonazo waigizaji wa filamu ulizoziona.

Wapo waliotamani kuwa “Batman” na wengine “Superman” na hata “Spider man” huku baadhi ya wanawake wakitamani kuwa “Wonder woman” ama “Cat woman”.

Endapo leo hii atatokea mtu na kukueleza kuwa ana kidonge ambacho ukikimeza, kinakupa nguvu mbadala kwa dakika tano, wewe ungependa upate nguvu ipi?

Hiyo ndiyo hali iliyopo kwenye filamu ya “Project Power” ambayo inatarajiwa kutimba kwenye mtandao wa Netflix ifikapo Agosti 14 mwaka huu.

Ukitumia kidonge hicho, hata risasi inaweza isipiteilimradi tu iwe ndani ya dakika tano. Picha| Looper.

Tulia, ipo hivi

Art (Jamie Foxx) anaungana na polisi kukiwinda kikundi ambacho kinatengeneza vidonge vinavyowapatia watu dakika tano za kuwa na nguvu mbadala. 

Siyo kutunisha misuli, La hasha!, naongelea nguvu za kutokuonekana, nguvu za kupiga ngumi za maana na nguvu za kasi ya ajabu.


Zinazohusiana


Hata hivyo, safari ya Art siyo kuwatafuta watengenezaji wa dawa hiyo pekee bali kumuokoa mtoto wake ambaye ametekwa na wahalifu hao.

Hapo ndipo anaungana na Frank (Joseph Gordon-Levitt) pamoja na mwanadada Robin (Dominique Fishback) kukamilisha mawindo yao.

Je wataweza kuwakabili watu walioshiba vidonge vya kuongeza nguvu huku wengine wakiwa na uwezo wa kutema moto? 

Kama umelipia kifurushi chako, Fuatilia filamu hii itokapotoka na ujionee mkono unavyochapwa baina ya nguli wa filamu na nyota wengine wakiwemo Newt (Machine Gun Kelly), Biggie (Rodrigo Santoro) na mwana mieleleka Luke Hawx (Oren Hawxhurst).

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
WORD BANK: Tanzania haina upungufu wa ajira, changamoto tija yake

WORD BANK: Tanzania haina upungufu wa ajira, changamoto tija yake

Nukta TV

CEOs kung'oka baada ya miaka 10, BoT yarudisha mjadala

CEOs kung'oka baada ya miaka 10, BoT yarudisha mjadala

Nukta TV

Onyo la wachumi ikiwa ukomo wa miaka 10 hautoondolewa kwa CEOs wa benki

Onyo la wachumi ikiwa ukomo wa miaka 10 hautoondolewa kwa CEOs wa benki

Nukta TV