Programu ya muziki ya Apple yaingia Tanzania

April 21, 2020 1:45 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • App hiyo imeingia katika nchi 17 za Afrika ikiwemo Tanzania.
  • Itawapa fursa watumiaji wa simu za iPhone kuburudika na muziki tofauti. 
  • Ni fursa kwa wanamuziki kunufaika na jukwaa hilo. 

Dar es Salaam. Kampuni ya Apple ya Marekani imetangaza nchi 17 za Afrika ikiwemo Tanzania ambazo zitaanza kufaidika na programu tumishi (App) ya Apple Music ambayo inawawezesha watu kupakia na kusikiliza muziki wakiwa mtandaoni. 

Baadhi ya wamiliki wa simu za iPhone walikuwa hawapati huduma hiyo kwa sababu duka la mtandaoni la App Store la kampuni hiyo lilikuwa halina bidhaa hiyo katika nchi zao. 

Ni dhahiri kuwa wapenzi wa muziki wana kila sababu ya kutabasamu kwa sababu wanaweza kuipata programu hiyo katika simu zao janja na kujivinjari kwa kila aina ya muziki. 

Apple katika taarifa yake iliyotolewa leo (Aprili 21,2020) imetaja nchi 17 za Afrika ambazo zimeongezwa kwenye orodha yake ya huduma hiyo ikiwemo Tanzania.

Nchi nyingine ni Malawi, Mali, Mauritania, Msumbiji, Namibia, Congo DRC Senegal, Ushelisheli, Sierra Leone, Algeria, Angola, Benin, Chad, Liberia, Madagascar na Tunisia.

“Tunayo furaha kusogeza huduma pendwa za Apple kwa watumiaji wa nchi nyingi kuliko hapo awali,” amesema Makamu wa Rais wa Apple Music na  na maudhui ya kimataifa wa kampuni hiyi, Oliver Schusser.

Amesema anaamini wamesogeza huduma zao karibu na wateja wao ili wafurahie ulimwengu wa muziki.


Zinazohusiana


Nje ya bara la Afria, Apple Music imeongezeka kwenye nchi za Kuwait, Qatar, Yemen, Croatia, Iceland na Macedonia Kaskazini.

Kwa muujibu wa Apple huduma hiyo inalipiwa kwa kipindi cha mwezi mmoja kwa Sh23,200 kifurushi binafsi na Sh34,700 kwa kifurushi cha familia ya watu sita.

Mbali na Apple Music, Apple imeingiza sokoni bidhaa zake zingine za  App Store, Apple Arcade, Apple Podcasts na iCloud kwa baadhi ya nchi za Afrika za  Cameroon,Ivory Coast, Congo DRC, Gabon, Libya, Morocco, Rwanda na Zambia.

Kwa Watanzania wanaotarajia kunufaika na Apple Music watafurahia huduma hiyoo kupitia teknolojia za kampuni ya Apple yaani kompyuta za Mac, Ipod na simu za iphone.

Pia ni fursa kwa wanamuziki kuuza nyimbo zao na kutanua wigo wa mashabiki  kupitia jukwaa hilo la watumiaji wa simu za iPhone.

Enable Notifications OK No thanks