NMB yalamba zaidi ya 79 bilioni China kuinua biashara ndogo na za kati

November 6, 2026 10:43 am · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Wafanyabiashara hao sasa wanapata fursa ya kupata mikopo itakayowawezesha kuongeza mitaji, na kuimarisha uwezo wa biashara zao kukabiliana na changamoto za kiushindani. 

Dar es Salaam. Benki ya biashara ya NMB PLC imepata mkopo wa Dola za Marekani milioni 30 sawa na zaidi ya 79 bilioni kutoka Benki ya Maendeleo ya China (CDB) kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa mitaji kwa biashara ndogo na za kati (SMEs) nchini Tanzania. 

Makubaliano hayo yametiwa saini jana Novemba 5, 2026 Makao Makuu ya NMB jijini Dar es Salaam, yakilenga kuchochea ukuaji wa biashara na kuimarisha ushirikiano wa kifedha kati ya Tanzania na China.

Akizungumza katika hafla hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, amesema fedha hizo zitaongeza uwezo wa benki kufadhili wafanyabiashara wanaohitaji mitaji ya kupanua shughuli zao. 

NMB ambayo imetambuliwa na jarida la Global Finance kuwa Benki Bora kwa Biashara Ndogo na za Kati Tanzania mwaka 2026 ni kwa zaidi ya mara sasa kwa mwaka huu inachukua mkwanja kwa ajili ya kuchagiza biashara hizo. Picha | NMB PLC

Ameongeza kuwa upatikanaji wa fedha ni muhimu katika kukuza biashara, kuongeza uzalishaji na kuchochea ajira nchini pamoja na kuimarisha huduma za kifedha kwa wafanyabiashara wanaofanya biashara na China. 

“Kupitia mfumo wa CIPS, NMB inatoa huduma za malipo kwa sarafu ya China (RMB), akaunti za biashara na ufadhili wa biashara za kimataifa, ikiunganisha wafanyabiashara wa Tanzania na wazalishaji wa China kupitia maonesho ya Canton Fair, amesema Zaipuna.

Shangwe wafanyabiashara wadogo, wa kati

Makubaliano kati ya NMB na CDB yanakuja wakati wafanyabiashara wadogo na wa kati nchini wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya mitaji, jambo linalo sababisha kudumaa kwa shughuli zao, na kupunguza uwezo wao wa kukua na kuchangia kikamilifu katika uchumi wa nchi. 

Kupitia makubaliano hayo, wafanyabiashara hao sasa wanapata fursa ya kupata mikopo itakayowawezesha kuongeza mitaji, kupanua shughuli zao, kuongeza uzalishaji na kuimarisha uwezo wa biashara zao kukabiliana na changamoto za kiushindani. 

Wafanyabiashara wadogo na wakati sasa wanapata fursa ya kupata mikopo itakayowawezesha kuongeza mitaji, na kuimarisha uwezo wa biashara zao kukabiliana na changamoto za kiushindani. Picha | NMB PLC

NMB ambayo imetambuliwa na jarida la Global Finance kuwa Benki Bora kwa Biashara Ndogo na za Kati Tanzania mwaka 2026 ni kwa zaidi ya mara sasa kwa mwaka huu inachukua mkwanja kwa ajili ya kuchagiza biashara hizo.

Zaipuna amebainisha kuwa licha ya kuongeza fursa za mitaji kwa wajasiriamali, makubaliano hayo yanakwenda kuimarisha biashara kati ya Tanzania na China hatua inayokwenda kuunga lengo la uchumi wa Dola za Marekani trilioni moja ifikapo 2050 kwa mujibu wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
6 Nov, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
6 Nov, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
BEI YA MAFUTA DAR | Sh10,000 kununua lita 2.44 za petroli, 2.42 za dizeli

BEI YA MAFUTA DAR | Sh10,000 kununua lita 2.44 za petroli, 2.42 za dizeli

Nukta TV

Namna Rais Samia alivyoshiriki kwenye Uchaguzi Mdogo, Jimbo la Chamwino

Namna Rais Samia alivyoshiriki kwenye Uchaguzi Mdogo, Jimbo la Chamwino

Nukta TV

Ndejembi: Wanachamwino wameona kwa macho, mrithi wangu ataendeleza kasi ileile

Ndejembi: Wanachamwino wameona kwa macho, mrithi wangu ataendeleza kasi ileile

Nukta TV