Ndiyo! mama aliyeambukizwa Corona anaweza kumnyonyesha mtoto wake

July 9, 2020 7:41 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Anashauriwa kuchukua tahadhari zilizoainishwa ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa na kunawa mikono.
  • Pia, sehemu ambazo mama huyo amezishika, zinatakiwa kusafishwa mara kwa mara kwa kutumia vitakasa (sanitizers).

Dar es Salaam. Ugonjwa wa corona umeibua sintofahamu nyingi na kufanya watu kuhoji kama kila wanachokifanya hakitawaweka wao au wale wawapendao kwenye hatari ya kuambukizwa ugonjwa huo aina ya COVID-19. 

Kati ya sintofahamu hizo ni ya mama anayenyonyesha kama anaweza kufanya hivyo pale anapogundulika kuwa ana COVID-19.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema hadi sasa hakuna utafiti unaoonyesha kuwa maziwa kutoka kwa mama mwenye COVID-19 yanaweza kumuambukiza mtoto pale anaponyonya maziwa hayo.


Zinazohusiana


“Hakuna sababu ya kuepuka au kuacha kunyonyesha,” imeeleza WHO. 

Hata hivyo, WHO imesema ili kujiweka salama, mama anayenyonyesha anakiwa kuchukua tahadhari muhimu za kumkinga mtoto wake dhidi ya ugonjwa huo ikiwemo kunawa mikono na maji tiririka na sabuni mara kwa mara kabla na baada ya kumnyonyesha mtoto.

Pia, mama anatakiwa kuvaa barakoa pale anapokuwa ananyonyesha na kutumia tishu anapopiga chafya na kuzitupa mahali salama. 

Pamoja na hayo, sehemu zote ambazo mama huyo anakuwa amezishika, zisafishwe mara kwa mara kwa kutumia vitakasa (sanitizers).

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
WORD BANK: Tanzania haina upungufu wa ajira, changamoto tija yake

WORD BANK: Tanzania haina upungufu wa ajira, changamoto tija yake

Nukta TV

CEOs kung'oka baada ya miaka 10, BoT yarudisha mjadala

CEOs kung'oka baada ya miaka 10, BoT yarudisha mjadala

Nukta TV

Onyo la wachumi ikiwa ukomo wa miaka 10 hautoondolewa kwa CEOs wa benki

Onyo la wachumi ikiwa ukomo wa miaka 10 hautoondolewa kwa CEOs wa benki

Nukta TV