Mifumo ya kidijitali itakayowavusha wafanyabiashara 2020

January 7, 2020 11:00 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Wanashauriwa kuwekeza katika programu tumishi zitakazowasaidia kupanga mipango, bajeti, kutanua soko na kuwahudumia wateja kwa urahisi zaidi.
  • Ni njia rahisi ya kuwafikia wateja popote walipo na wakati wowote. wateja sokoni.

Dar es Salaam. Mwaka umeanza na huenda ukawa umejiwekea malengo makubwa zaidi  ya namna ya kuboresha na kuikuza katika biashara yako kwa kutumia mifumo mbalimbali ya teknolojia ili kukua kiuchumi.

Mchango wa teknolojia katika shughuli mbalimbali za uchumi kwa sasa ni mkubwa kwani watu wengi wamehamia zaidi mtandaoni na njia mbalimbali za kukuza biashara ni kwa kutumia teknolojia zinazotumika na watu kila siku. 

Hii ni baadhi ya mifumo ya dijitali inayoweza kutumiwa na wafanyabiashara mwaka 2020 kuwafikia watu wengi ili kuwauzia bidhaa na huduma:

  1. Tumia maduka ya mtandaoni

Ikizingatiwa kuwa watu wengi wanapatikana mtandaoni, ni wakati muafaka kwa biashara yako kuipeleka mtandaoni ili kufaidika na soko kubwa lisilo na mipaka. 

Maduka hayo yanayoendeshwa na programu tumishi za simu (Apps) yanawawezesha mfanyabiashara na mteja kuwasiliana kwa kuoneshana bidhaa mtandaoni, kufanya manunuzi na kupata maoni ya namna gani mfanyabiashara anaweza kuboresha huduma na bidhaa mtandaoni.

Maduka unayoweza kuuza bidhaa na huduma ni pamoja na Kikuu, Google My Business,  ebay, Amazon kutoka Marekani na nyingine nyingi zinazohusisha mawasiliano ya moja kwa moja kati ya mteja na muuzaji kuhusu bidhaa mbalimbali. 

  1. Matumizi ya mitandao ya kijamii

Matumizi ya mitandao ya kijamii ni mfumo mwingine muhimu unaohusisha teknolojia ya simu kwa kutangaza bidhaa kwenye mitandao ya kijamii na mwishoni kupata wateja kupitia matangazo na soko ulilonalo mtandaoni. 

Baadhi ya mitandao inayotumika sana katika utangazaji na masoko ni pamoja na Instgram, WhatsApp na Facebook, Kwa programu hizi, fanyabiashara ana unwezo wa kuonyesha bidhaa yake na kupata wateja kwa haraka na muda wowote kuliko akiwa sokoni anasubiri wateja.                                      Inasaidia bidhaa kujulikana haraka kuliko ikisubiri wateja sokoni. Picha |Mtandao.

  1. Programu tumishi za kufanya mipango ya biashara.

Mfanyabiashara yoyote anahitaji mipango mikakati inayoweza kumwongoza katika kufanya maamuzi mbalimbali kwenye biashara yake. 

Zipo programu tumishi mbalimbali kama “Business Plan Quick Builder” na “Business Plan” zinazoweza kuwasaidia kwa asilimia kubwa wafanyabiashara kutengeneza mipango ya biashara inayotekelezeka.

  1. Pakua programu tumishi kwa ajili ya bajeti

Kupanga bajeti katika biashara ni suala muhimu kwa sababu bila mpangilio mzuri wa mahesabu huenda biashara ikapata hasara na kushindwa kuendelea. 

Elimu kuhusu namna ya kutengeneza bajeti na  inavyoweza kusaidia katika ujasiriamali pia zinapatikana katika programu tumishi mbalimbali ikiwemo ya  “Monthly Budget Planner”, “My Budget rganizer” na “Money Manager” zinazosaidia kujua ni namna gani unaweza kupangilia mapato na matumizi katika biashara kwa ufasaha.


Zinazohusiana:


Teknolojia hizi zina umuhimu gani kwa mfanyabishara?

Kwa mfanyabiashara zinamfungulia fursa ya soko kubwa zaidi kuliko akisubiri wateja kwenda sokoni kuangalia biashara yake.

Mfanyabiashara wa nguo na viatu jijini Dar es Salaam, Neema Gerald ameiambia www.nukta.co.tz  ameanza kutumia mitandao ya kijamii kwenye biashara yake mwishoni mwa mwaka jana na imempa faida kubwa kuliko kusubiri wateja dukani kufanya manunuzi.

“Kupitia mitandao ya kijamii nimepata wateja wengi kuliko wale niliokuwa nikiwaalika dukani. Na hii imenipa nguvu ya kutumia mitandao ya kijamii zaidi ya kukaa na kusubiri wateja dukani,” amesema Neema.

Enable Notifications OK No thanks