Mate, jasho la mgonjwa aliyepona havisambazi virusi vya Ebola

January 14, 2023 7:03 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • WHO wasema mgonjwa aliyepona Ebola hasambazi virusi hivyo.
  • Hata hivyo, bado kuna ulazima wa kuchukua tahadhari juu ya gonjwa hilo.

Dar es Salaam. Hata wakati makali ya ugonjwa wa Ebola yakiendelea kupungua kwenye nchi nyingi zilizokumbwa na ugonjwa huo ikiwemo Uganda, bado taarifa za uzushi kuhusu ugonjwa huo zinaendelea kusambazwa na kuathiri watu.

Moja ya uzushi huo ni mate na  jasho la mgonjwa aliyepona Ebola kusambaza virusi vya ugonjwa huo, jambo halina uthibitisho wa kitabibu.

Kwa mujibu wa Daktari Patrick Otim Ramadan kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) Ofisi ya kanda ya Afrika, mate, jasho na damu ya mgonjwa aliyepona Ebola haviwezi kusambaza virusi hivyo.

“Mpaka mgonjwa wa Ebola akiruhusiwa kutoka wodini inamaanisha virusi havipo tena kwenye damu hivyo haviwezi kurudi kwenye mate au jasho,” amesema Dk Ramadhan.

Kwa wakati huo wanafamilia na jamii inayomzunguka mgonjwa huyo aliyekwisha kupona hawapo tena kwenye hatari ya kupata maambukizi mapya ya ugonjwa huo, kinyume na uzushi unaoendelea kusambazwa.

Hata hivyo, ikiwa mgonjwa wa Ebola ambaye bado hajapona vizuri au bado anaumwa anaweza kueneza vizuri hivyo kwa watu walio karibu naye kupitia damu, mate au jasho.

“Mtu ambaye bado anaumwa Ebola yupo kwenye hatari ya kuwaambukiza wengine na wala siyo mgonjwa aliyepona kama inavyoaminika,” amesema mtaalam huyo. 


Soma zaidi:


Njia za kujikinga na Ebola

Ili kuzuia maambukizi ya Ebola, WHO inawataka wahudumu wa afya kuvaa vifaa vya kujikinga wakati wa kumuhudumia mgonjwa wa Ebola pamoja na kuosha mikono baada ya kumuhudumia mgonjwa au kumtembelea.

​Kuepuka kula nyama ambayo haijapikwa vizuri, kula nyama mbichi au mizoga na kugusa wanyama wenye maambukizi.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
25 Sep, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
26 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Lissu alivyotumia saa tisa kujitete mahakamani, aibua hoja tatu nzito

Lissu alivyotumia saa tisa kujitete mahakamani, aibua hoja tatu nzito

Nukta TV

Walimbwende ‘Miss World’, kupewa makabila Tanzania kuwakilisha kimataifa

Walimbwende ‘Miss World’, kupewa makabila Tanzania kuwakilisha kimataifa

Nukta TV

Makonda: Jezi ya Taifa Stars mbaya, hangaikeni  iwe nzuri

Makonda: Jezi ya Taifa Stars mbaya, hangaikeni iwe nzuri

Nukta TV