Kutana na Gugu: Bata mwanafunzi aliyesajiliwa chuo kikuu China

August 13, 2018 7:54 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Gugu azua gumzo kwenye mitandao ya kijamii.
  • Mmiliki wa Gugu afurahia kukwepa gharama za kumtunza.
  • Chuo hicho kinasifika kwa kudahili wanyama kama wanafunzi wengine.

China. Katika hali isiyo ya kawaida, Chuo Kikuu cha Shanghai Maritime cha China kimekubali kumdahili bata mzinga kuwa mwanafunzi ambaye atakuwa anaishi chuoni hapo ikiwa ni sehemu ya kuthamini wanyama..

Uamuzi huo ulifikiwa Agosti 10 mwaka huu, baada ya mmliki wa bata huyo ambaye alitumia mtandao wa Weibo ambao unafanana na Twitter kupenyeza maombi yake ili bata mzinga wake anayejulikana kwa jina la ‘Gugu’ asajiliwe na kuwa sehemu ya wanafunzi wa chuo hicho.

Mmiliki wa Gugu ambaye anaishi katika mji wa Songjiang anasema hatamtunza tena bata mzinga wake kwa sababu chuo kimekubali kumchukua na kuanzia sasa atakuwa anaishi chuoni.

Gugu akiwa kwenye moja maeneo ya kutunzia wanyama chuoni Shangai Maritime. Picha|cgtn.com

Kwa mujibu wa Shirika la Habari CGTN uongozi wa chuo hicho umesema Gugu mwenye mwaka mmoja atakuwa sehemu ya bata wengine ambao wanawatunza kwenye ziwa dogo ikiwa ni sehemu ya kivutio kwa watu wanaotembelea chuo hicho.

Kutokana na mapenzi ya chuo hicho kwa wanyama kimefungua akaunti ya Weibo maalum kwa bata mzinga ambapo ujio wa Gugu umeongeza idadi ya watu wanaoifuta akaunti hiyo na kufikia zaidi ya wafuasi 6,000. 

Watumiaji wa mtandao wamekisifu chuo hicho kwa uamuzi wake wa kukubali maombi ya wanyama ambao wanadahiliwa chuoni hapo kama jambo la mfano ambalo vyuo vingine vinapaswa kuiga katika kuwajali wanyama. 

 Kwa vyuo vya China sio jambo la kushangaza kukutana na akaunti za mitandao ya kijamii za wanyama. Mathalani Chuo Kikuu cha Zhejiang Gong Shang kilichopo jimbo la Mashariki mwa Zheijiang kimevutia watu wengi kwa mtindo wake wa kuweka milio ya nguruwe ambao wanafugwa chuoni katika akaunti yake ya Weibo.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW