Kicheko, maumivu: Wanunuzi wa viazi mviringo Lindi, Njombe

March 16, 2020 10:44 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Bei inayotumika leo Lindi ni mara nne zaidi ya Njombe, jambo linalowafaidisha zaidi wafanyabiashara ambao wamepeleka viazi mviringo mkoani humo. 
  • Gunia la kilo 100 la viazi mviringo katika masoko ya mkoani Lindi  linauzwa kwa Sh120,000, wakati masoko ya Njombe linauzwa kwa Sh30,000.

Dar es Salaam. Watumiaji wa viazi mviringo hasa kutengeneza chipsi katika Mkoa wa Lindi leo watalala na maumivu kutokana na bei ya gunia la kilo 100 la zao hilo kuuzwa mara nne zaidi ya bei inayotumika katika Mkoa wa Njombe. 

Takwimu za mazao makuu ya chakula zilizotolewa na WIzara ya Viwanda na Biashara  leo (Machi 16, 2020) zinaeleza kuwa gunia la kilo 100 la viazi mviringo katika masoko ya mkoani Lindi  linauzwa kwa Sh120,000, wakati masoko ya Njombe linauzwa kwa Sh30,000.

Hiyo ina maana kuwa bei inayotumika leo Lindi ni mara nne zaidi ya Njombe, jambo linalowafaidisha zaidi wafanyabiashara ambao wamepeleka viazi mviringo mkoani humo. 

Bei hiyo inayotumika Lindi ndiyo bei ya juu huku ya Njombe ikiwa ni ya chini ikilinganishwa na bei zinazotumika katika maeneo mengine nchini. 


Soma zaidi: 


Hata hivyo, takwimu hizo zinaonyesha kuwa maharage ndiyo yanauzwa bei ghari leo sokoni ambapo bei ya juu imerekodiwa katika soko la Tandika, Temeke jijini Dar es Salaam. Gunia la kilo 100 linauzwa kwa Sh270,000. Bei ya chini ya maharage ni Sh90,000 katika mkoa wa Rukwa. 

 Mazao makuu ya chakula hujumuisha mchele, maharage, viazi mviringo, mahindi, mtama, uwele, ulezi na ngano.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW