Kampuni zinazowapa wanawake fursa za uongozi huvuna faida kubwa: Ripoti

May 25, 2019 10:11 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link

Jamii bado ina kibarua kigumu cha kuhimiza taasisi na kampuni kuongeza idadi ya wanawake katika nafasi za juu za uongozi ili kupata mfanikio yaliyotajwa katika ripoti hiyo. Picha|Mtandao.


  • Ripoti mpya ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) zinapata ongezeko la faida kati ya asilimia tano hadi 20 kutokana kushirikisha wanawake.
  • Uwiano wa jinsia katika kampuni unaongeza pia ubunifu na uwazi.
  • Lakini changamoto za elimu na utamaduni wa kiume katika kampuni unakwamisha wanawake kupata nafasi nyingi zaidi.

Dar es Salaam. Ripoti mpya ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) iliyotolewa katikati ya wiki hii imebaini kuwa kampuni za kibiashara zenye uwiano mzuri wa  jinsia kwa kuwapa fursa sawa wanawake na wanaume katika ngazi ya juu ya uongozi zinafanya vizuri katika shughuli zao ikiwemo kupata faida kubwa.

Ripoti hiyo ya  Wanawake katika Biashara na Usimamizi ni matokeo ya utafiti wa takribani kampuni 13,000 katika nchi 70 ambapo zaidi ya asilimia 57 ya washiriki wa utafiti huo walikubali kuwa uwepo wa jinsia tofauti uliboresha matokeo ya biashara katika kampuni zao. 

“Takribani robo tatu ya kampuni zenye mchanganyiko wa viongozi ziliripoti ongezeko la faida kati ya asilimia tano hadi 20, wengi wao wakishuhudia ongezeko kati ya asilimia 10 na 15,” inasomeka sehemu ya ripoti hiyo. 

Ripoti hiyo ambayo ilizinduliwa Mei 22, 2019, Geneva, Uswisi inaeleza zaidi kuwa ufanisi wa uwiano wa kijinsia unaimarisha sifa za kampuni hasa kama ina uwezo wa kuvutia na kuendeleza wafanyakazi wenye vipaji, ubunifu na wa wazi katika kutekeleza majukumu yao. 

“Takribani asilimia 57 (zaidi ya nusu) walisema ilikuwa rahisi kuvutia na kutunza vipaji huku zaidi ya asilimia 54 walisema waliona maboresho katika ubunifu, uvumbuzi na uwazi na pia idadi hiyo ilieleza kuwa ufanisi wa uwiano wa kijinsia uliimarisha sifa za kampuni zao,” inaeleza ripoti hiyo.

Hata hivyo, ripoti hiyo inasema faida ya uwiano mzuri wa kijinsia inaanza kuonekana pale ambapo wanawake wanashikilia asilimia 30 ya ngazi za juu za uongozi. Lakini takribani asilimia 60 ya makampuni hayafikii lengo hilo.


Zinazohusiana:


Jamii bado ina kibarua kigumu cha kuhimiza taasisi na kampuni kuongeza idadi ya wanawake katika nafasi za juu za uongozi ili kupata mfanikio yaliyotajwa katika ripoti hiyo. 

Machi 8, 2018, gazeti la The Citizen lilipoti kuwa asilimia nane tu ya wanawake nchini ndiyo wanashikilia nafasi za juu za uongozi yaani Wakurugenzi Wakuu (CEO) katika sekta ya fedha ambapo asilimia zinazobaki ni wanaume. 

Mkurugenzi wa Idara ya ajira ya ILO, Deborah France-Massin akizungumzia ripoti hiyo, amesema wanaume wengi wanawabana wanawake kupenya kwa sababu ya elimu na utamaduni zaidi wa kiume katika kampuni. 

“Ninafikiri pia elimu ya wanawake katika siku za nyuma, na hata sasa bado ni wanawake wachache wanaenda katika masomo ya sayansi na teknolojia, pia wanawake wachache wanasomea masuala ya uchumi au uzalishaji bidhaa,” amesema Massin wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
18 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
18 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
18 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Nukta TV

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Nukta TV

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Nukta TV