“Just Mercy”: Filamu ya machungu ya walioonewa gerezani

February 28, 2020 11:53 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link

McMillan Mmarekani mweusi anahukumiwa kifo baada ya tuhuma za kumuuwa binti wa kizungu. Picha| Roger Ebert.


  • Inaelezea jinsi wanyonge wanavyotaabika kwa kukosa wawakilishi bora mahakamani.
  • Michael Jordan, Jamie Foxx na wengine lukuki wameshiriki kwenye filamu hii inayosimulia kisa cha kweli.
  • Mafunzo ya filamu hii yanamfaa kila mwanasheria.

Dar es Salaam. Hakika ni wiki ndefu lakini lazima ifike mwisho na mambo mengine yaendelee. Tunapoanza wikiendi leo, unahitaji mapumziko kwa  ajili ya kujiweka tayari kuianza wiki nyingine kwa kishindo.

Unaweza kufurahia mapumziko yako kwa kutazama filamu zinazoonyeshwa katika kumbi za kuangalizia filamu za Century Cinemax zilizopo kwenye maduka makubwa yakiwemo ya Milmani city na Mkuki house.

Nini kimeandaliwa kwa ajili yako? 

Ni muda muafaka wa kumtazama Michael Jordan ambaye amerudi jukwaani kupitia filamu ya “Just Mercy” akiwa na nguli Jamie Foxx pamoja na Brie Larson.

“Just Mercy” inamhusu  Bryan Stevenson (Michael Jordan), mhitimu wa masomo ya sheria kutoka Chuo Kikuu cha Havard cha nchini Marekani  mwenye malengo ya kutoa msaada wa kisheria kwa wanyonge walioonewa.


Zinazohusiana


Ni maamuzi magumu lakini hii ndiyo safari yake.

“Nieleze kila kitu kilichotokea,” ni Stevenson akiongea na Walter McMillian (Foxx) ambaye yupo gerezani akitumikia hukumu yake kwa makosa ya uuaji.

McMillian ambaye ameshajikatia tamaa na maisha yake hana imani kama kijana mdogo kama Stevenson anaweza kubadilisha maisha yake baada ya kuhukumiwa kifo kwa kusingiziwa kumua binti wa kizungu mwenye miaka 18.

Licha ya kujua kwamba safari yake ya kufuatilia kesi hiyo itakasirisha watu wengi, Stevenson anashirikiana na wakili Eva Ansley (Larson) kufufua vidonda vilivyokuwa vimepona.

Nini kitaendelea? Fuatilia filamu hii iliyoongozwa na Destin Cretton ikisimulia kisa cha kweli kwa gharama ya Sh10,000 katika kumbi za sinema jijini Dar es Salaam.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW