Jinsi ya kujenga hisia juu ya ‘Brand’ ya biashara yako

February 19, 2019 12:29 pm · Charles
Share
Tweet
Copy Link
  • Kujenga hisia ni kufikia mahitaji na matarajio ya mteja wa bidhaa au huduma zako.
  • Mteja anaanza kukununua kwenye lugha unayotumia, mwonekano wako binafsi na mazingira yako unayotolea huduma yako kabla hajanunua bidhaa yako.
  • Mfanye mteja kuwa sehemu ya familia ya biashara yako ili kujenga mahusiano mazuri.

Maana ya ‘brand’ kwenye biashara ni kile ambacho mteja anakumbuka na kukijua kuhusubidhaa au huduma yako. 

Lakini ni zaidi ya hapo, brandni lazima itibu hisia za mteja kwa kuhakikisha inagusa na kufikia matarajiio ya kihisia ya mteja juu huduma na biashara zetu kwa ujumla. 

Mathalani, mimi ninachokikumbuka kuhusuNuktani taasisi yenye mpangalio na watu makini yamkini hii ndiyo brand yao ya kibiashara sasa wanaendeleaje kuwa hapa ambapo mimi ndiyo nawafahamuna mwisho wa siku kila mteja akifika kwao mahitaji yake yatakuwa ni kupata mguso wa kihisia(now days people do not buy LOGIC, they buy EMOTIONS).

Swali la msingi kwa kila anayefanya biashara, ni kitu gani unamfanyia mteja wakochenye kuleta utofauti wenye tija? Ukiweza kulijibu swali hili la msingi unakuwa umepiga hatua kubwa sana. Unawezaje kumfanya mteja wako ajisikie kujaliwa na kupewa kipaumbele kwenye mahitaji yake?

Kuna baadhi ya njia za kuzingatia katika kuhakikisha hisia za mlaji/mteja zinakua juu na ili kuipaisha brand yako;

Matumizi mazuri ya lugha

Mteja anatamani kusikia lugha ya shukrani, anatamani kusikia lugha ya unyenyekevu, lugha ya kukumbushwa, lugha ya maelekezo, lugha ya kumsifia na kumjali, lugha ya kueshimiwa na kupewa kipaumbele kwanza.

Mahusiano yetu hujengwa na lugha zetu na pia huvunjwa na lugha zetu, kwa namna gani unatumia lugha inakupa nafasi kubwa ya kukidhi mahitaji ya mteja wako kuhakikisha unamshukuru mteja wako ili ajisikie vizuri na aamini bila ya huduma ya hawezi kuishi. Kilabinadamu yeyote anatamani kuzisikia sauti hizimasikionimwake. 

Na kwenye lugha si sauti tu lakini hata mwonekano wako lazima mtoa huduma tabasamu liwe la kudumu usoni mwako.

Kanuni ya kufanikiwa katika biashara ni kumsikiliza mteja wako na kutumia lughaya upole ili kujenga mahusiano mazuri ya kibiashara. Picha|Energy Change Lab.

Mazingira ya biashara

Watejawako wanakula pia hata mazingira yako ya kazi kwa sababuhisia hujengwa pia kwa kuona na kusema. 

Mteja anaweza kutembelea biashara yako na akasema kama huyu mazingira yake ni machafu kwa kiasi hiki je? hii bidhaa yake anayoniuzia  iko na hali gani au imetengenezwa kwenye mazingira yapi, hapa unashusha hisia za mlaji lazima ujifunze kuweka mazingira yenye kuakisi kile unachokifanya au kukiuza.


Soma zaidi:


Hali ya mtoa huduma

Kwenyebranding tunasema “customers they do not buy products/services they buyYOU” walaji hawanunui bidhaa au huduma unayoitoa bali wanakununua wewe unayoitoa huduma husika.

Mteja anaanza kukununua kwenye lugha unayotumia, mwonekano wako binafsi na mazingira yako unayotolea huduma yako. 

Wekeza kuhakikisha mteja anajisikia vizuri kwa kumpa attention (muitikio)ya kutosha, mpe zawadi, mshukuru, tambua mchango wake hata kwa kusema tu au kumwandika ujumbe ufupi.

Mpe nafasi ya kutoa maoni kuhusubiashara, mshikirishe kwenye vitu vingine kama inawezekana kwani hii itakusaidia kujenga mahusiano mazuri, zaidi ya yeye kuwa mteja tu na hapa utakuwa ni mwanafamilia wa biashara yako.

Mpe mteja nafasi ya kuwa sehemu ya familia ya biashara yako. Hii itakusaidia kuimarisha mahusiano yenu na kupata faida iliyokusudiwa. Picha|Energy Change Lab. 

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW