JIFUNZE JINSI MKATE UNAVYO OKWA CHINI YA ARDHI

November 20, 2017 3:52 am · Daniel
Share
Tweet
Copy Link

 Mkate  uoko kwenye jiko la oveni au kwa njia ya kawaida kwa kutumia mkaa,nchini Iceland ni tofauti kabisa,    mkate huokwa  chini ya ardhi kisha  kutumika kama kifungua kinywa na  bado watu wakausifia kwa utamu wake.

Mikate hiyo ambayo inaokwa chini ya ardhi inayojilikana kama  radi kwa tasfri isiyo rasmi lakini  maarufu kama Hverabraou ama thunder bread mikate hiyo ambayo huokwa kwenye chemichemi ya moto (geothermal springs) ni yenye rangi za weusi weusi kwa mbali na brauni na migumu kiasi na mitamu sana.

​

Mkate wa radi ni jina la utani tu,mkate huo jina lake  halisi ni mkate wa chemchemu katika tasfri isiyo rasmi  na katika lugha yao ikijulikana kama hverabrauo au hot-spring-bread.Mkate huo unaopikwa kwa mvuke unaotoka katika chemichemi chini ya ardhi.

Katika kila familia nchini Iceland wanajua jinsi ya kupika aina ya mkate huu maana ni sehemu yao ingawa wanatofautiana kidogo kwenye manjonjo au viungo na kila familia huisi mkate wake ni bora zaidi mkate huo huliwa karibia mwaka mzima nchini humo.

Mkate  wa chemichemi hupikwa kwa kuchanganya vikombe viwili vya sukari pamoja na lita moja ya maziwa , vikombe viwili vya unga, vikombe vinne rai,na kijiko kimoja cha chumvi.

Kisha mpikaji hutakiwa kuchanganya kwenye chombo cha bati (bakuli)  ilikupata huo mchanganyiko , hilo bakuli husaidia mkate usigandie wakati wakupika.Pia inatakiwa chombo hicho kikazwe na kisiwe chombo ambacho kinawezi kupitisha maji.

​

Baada ya maandalizi yote hayo  mpikaji wa mkate huo hutakiwa kuchimba shimo kwenye chemichemi kisha kuweka bakuli la bati  lenye  mchanganyiko nilio kwishaeleza hapo juu kwa muda wa siku moja au masaa 24  ili huo mkate uokwe vizuri.

Ikishapita masaa 24 ataweza kuufukua mkate  ambao utakuwa  tayari kwa kuliwa mkate huo  sio tu mnzuri machoni kwa maana ya kuvutia kwake lakini pia kwa utamu wake.

Tanzania nayo imebaraikiwa kwa kuwa na chemichemi kama ya Kikuletwa na nyinginezo ,swali lakujiuliza hapa je chemichemi hizo zina manufaa kiasi gani kwa jamii zinazozungua maeneo hayo na taifa kwa ujamla  kama sehemu za kitalii.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
21 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Nukta TV

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

Nukta TV