Hii ndiyo sababu inayoweza kuua biashara yako kwa haraka

February 10, 2020 9:12 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Sababu kubwa iliyopo ni kukosa kutoa huduma bora kwa wateja wako.
  • Ipe thamani biashara yako kwa kuwathamini na kuwajali wateja wako.

Dar es Salaam. Wafanyabiashara wenye ndoto ya kuendeleza biashara zao na kuhimili ushindani wa soko la bidhaa  wametakiwa kuimarisha mifumo ya kuwahudumia wateja wao kwa kuwathamini na kuwapa bidhaa bora. 

Siku zote tabia ya ununuzi ya wateja hubadilika, ni wajibu wa mfanyabiashara kujifunza mbinu za kufikia matarajio ya wateja wake na kutoa huduma zilizo bora kila wakati. 

Mchambuzi huru wa masuala ya biashara,  Nazareth Eliguard aliyekuwa akizungumza na Nukta (www.nukta.co.tz) amesema mfanyabiashara mzuri ni yule anayetambua umuhimu wa wateja wake kwani ndiyo wanaoipa biashara jina na wana uwezo wa kuinua biashara hiyo katika viwango anavyotaka. 

“Ukitoa huduma mbaya kwa mteja mmoja, kumbuka unaweza ukawa umeua soko la watu wengine 10 kwani wateja wana tabia ya kuambizana na mara baada ya kuambizana wanahama wote kwa pamoja,” amesema Eliguard.


Zinazohusiana:


Wapo baadhi ya wafanyabiashara waliofanikiwa sana, huridhika na mafanikio waliyoyapa hata kufikia hatua ya kujisahau kuwajali wateja wao, pasipo kujua huo ndiyo mwanzo wa anguko lao. 

Eliguard amesema hatua muhimu za kuchukuliwa na wafanyabiashara ni kujenga biashara kwa uangalifu kwa sababu siyo kazi rahisi kujua kila kitu anachopenda mteja wako, lakini mfanyabiashara anaweza kuweka jitihada za kuleta wateja kutokana na huduma bora anazotoa.

Amesema pamoja na matamanio ya kufanikiwa katika biashara, mfanyabiashara ana jukumu la kuongeza thamani ya bidhaa anayouza ili huduma ya mteja anayotoa iwe na maana zaidi.

Naye mwanafunzi anayesomea masuala ya biashara kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini kampasi ya Dar es Salaam (Tudarco), Emmanuel Asenga amesema kuwa kuna hatari ya biashara kufa mapema ni inatokea pale mfanyabiashara anaposhindwa kutambua kwamba wateja ulionao ni mali na kuwahudumia vile wanavyopaswa kuhudumiwa.

“Ukifanya biashara kwa mazoea lazima ife. Ukijua kuchukulia wateja wako kama “Asset” (mali) kamwe biashara haitoyumba ila ukifanya vinginevyo ni hatari kwani utafunga biashara mapema sana,” amesema Asenga.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV