Hapana: Messi hajaposti picha akiwa amevaa jezi ya klabu ya Yanga

January 12, 2022 8:03 am · Wilson
Share
Tweet
Copy Link
  • Picha yake imehaririwa na kumuonyesha kavaa jezi ya Yanga.
  • Hakuna taarifa rasmi kuhusu mchezaji huyo wa PSG kuvaa jezi ya Yanga.

Dar es Salaam. Kama wewe ni miongoni mwa watu ambao wamekutana na picha mtandaoni inayomuonyesha mchezaji wa PSG (klabu ya Paris Saint-Germain) Lionel Messi akiwa na familia yake huku wakiwa wamevaa jezi inayodaiwa ni ya klabu ya Young Africans (Yanga) na akaamini, fahamu kuwa umedanganywa.

Picha hiyo ambayo imetolewa katika moja ya mabandiko ya mtandao wa Twitter siyo ya kweli na imehaririwa ili kutimiza malengo fulani ikiwemo kupotosha umma.

Kwa kutumia zana za kidijitali ikiwemo TinEye na Google Image, timu ya NuktaFakti tumefanikiwa kugundua kuwa picha hiyo iliyopostiwa katika ukurasa wa Twitter wa samkicheko ikimuonyesha Messi pamoja na familia yake akiwa amevaa jezi ya Yanga ya Tanzania siyo kweli kwa kuwa imeghushiwa. 

Picha hiyo kwa mara ya kwanza ilianza kusambaa mitandaoni baada ya mtandao wa Twitter wa Goal  kuichapisha Desemba 29 mwaka jana.

Baadaye picha hiyo ilichapishwa tena Januari 2, 2022 na tovuti ya www.ole.com. 

Katika picha hizo mbili, Messi na familia yake hawajavaa jezi ya Yanga licha ya kuwa tisheti walizovaa zinafanana na jezi za timu hiyo. 

Hata hivyo, katika kurasa za mitandao ya kijamii na tovuti za klabu ya Yanga na mdhamini wake mkuu kampuni ya GSM hawajaweka taarifa yoyote rasmi kuhusu Messi kuvaa jezi zao.

Hiyo picha inayosambaa mtandaoni hasa Whatspp siyo ya kweli, imehaririwa. Usiendelee kuisambaza kwa watu wengine ili kuepuka upotoshaji.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV