Fahamu maeneo yatakayoipatia ‘mpunga’ bajeti ya nne ya Magufuli
- Katika bajeti hiyo ya mwaka 2019/20, Serikali inatarajia kukusanya Sh33.11 trilioni ikiwa ni ongezeko la takriban asilimia 2 kutoka makadirio ya bajeti ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 2019.
- Washirika wa Maendeleo wanatarajiwa kuchangia Sh2.78 ambayo ni sawa na asilimia 8 ya bajeti yote.
Dar es Salaam. Juni 13 mwaka huu, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisoma makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka wa fedha wa 2019/2020 ya Sh33.11 trilioni huku takriban asilimia 70 ya mapato hayo yakitoka vyanzo vya ndani.
Hii ni bajeti ya nne tangu Rais John Magufuli aingie madarakani Novemba 2015 akijikita zaidi katika uwekezaji wa uchumi wa viwanda.
Katika mwaka huo wa fedha unaoanza Julai, Dk Mpango alibainisha kuwa asilimia 63 ya mapato hayo yatatumika kwa ajili ya matumizi ya kawaida wakati kiwango kilichosalia zaidi ya theluthi au asilimia 37 kikitumika kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikiwemo reli ya kisasa ya viwango vya kimataifa (SGR) na ujenzi wa mradi wa umeme wa maporomoko ya maji wa Rufiji.
Ili Serikali ifanikishe azma yake, itakuwa na kazi ya kukusanya mapato kugharamia miradi hiyo. Picha hii chini inabainisha maeneo ambayo Serikali inatarajia kupata mapato yake katika mwaka wa fedha wa 2019/20.

Latest
