Daladala ni kila kitu usafiri Tanzania

January 23, 2019 6:04 pm · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni asilimia 85.7 ya mabasi yote yaliyopo nchini na hutumika zaidi kusafirisha abiria katika miji na vijiji.
  • Kwa kila daladala tano zilizopo Tanzania, moja ipo mkoa wa Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema Tanzania ina mabasi 49,000 ambapo kati ya hayo 7,000 ni mabasi yanayofanya safari zake mikoani na yanayobaki ambayo ni sawa na asilimia 85.7 ni daladala zinazofanya safari zake ndani ya miji. 

Katika hotuba yake ya Desemba 20, 2018 wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa daraja la kisasa la Salender litakalopita juu ya Bahari  ya Hindi na kupunguza adha ya foleni jijini Dar es salaam, alisema katika daladala zote zilizopo nchini, 9,000 zinapatikana mkoa wa Dar es Salaam, ambapo zikiwekewa mikakati mizuri zinaweza kuwa sehemu ya kukuza mapato ya Serikali. 

Kwa takwimu hizo, inamaanisha kuwa kwa kila daladala tano zilizopo Tanzania, moja ipo mkoa wa Dar es Salaam.

Kamwelwe alisema hadi mwishoni mwa Januari 2019 mabasi yote yanatakiwa kutumia mfumo wa utoaji wa tiketi za kielektroniki kwa abiria ili kurahisisha upatikanaji wa kodi ya Serikali.

Mwaka 2017 sekta ya uchukuzi ilikuwa ni moja zilizofanya vyema baada ya kuchangia asilimia 16.5 ya Pato la Taifa (GDP) ikiwa nyuma kidogo ya sekta ya utalii ambayo ilichangia asilimia 17.2.

 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV