Chatbot: Teknolojia inayosaidia ukuaji wa soko la bidhaa

- Ni programu ya kompyuta iliyotengezwa kwa ajili ya kuwezesha mawasiliano kati ya  binadamu na mashine.Â
- Ni njia rahisi ya kuimarisha mahusiano na wateja, kuboresha huduma na bidhaa.Â
Dar es salaam. Katika kuhakikisha kampuni au masharika yanaendelea kuuza bidhaa na kutoa huduma bora kwa wateja, teknolojia imekuwa kiungo muhimu cha kufanikisha mikakati ya kukuza soko.
Moja ya teknolojia hizo ni matumizi ya ‘chatbot’ ambayo imeanza kujipatia umaarufu kwa kampuni zinazohitaji kuimarisha mahusiano na mawasiliano na wateja wake ili kuhakikisha huduma zinapatikana saa 24 hata pasipo kuhitaji msaada wa mtu.Â
Chatbot ni programu ya kompyuta iliyotengezwa kwa ajili ya kuwezesha mawasiliano kati ya  binadamu na mashine.Â
Programu hiyo imekuwa fursa muhimu kwa ukuaji wa masoko ya kijigitali kwasababu mtu anaweza pata taarifa za masoko  kwa masaa 24 bila ya mwingiliano wa binadamu  kupitia tovuti na programu tumishi mbalimbali.
Ripoti ya Kongamano la masuala ya teknolojia la Gartner iliyotolewa mwaka 2011 inaeleza kuwa ifikapo  mwaka 2020 asilimia 80 ya biashara zitakuwa zinaendeshwa kwa sehemu kubwa na mashine (chatbots), jambo litakalopunguza kazi zinazofanywa na binadamu.
Zinazohusiana:Kutana na shangazi roboti wa Tanzania aliyepania kutokomeza mimba za utotoni
Kutokana na umuhimu wake, taasisi mbalimbali nchini zinatumia teknolojia hiyo ili kurahisisha mawasiliano na utoaji huduma katika maeneo yao.Â
Mathalan, benki ya  CRDB kupitia tovuti yake ina huduma inayojulikana kama ‘We are Online Let’s chat’;na benki ya Stanbic (Webchat).Â
Chatboat nyigine ni ‘eshangazi’ (shangazi wa kimtandao ) ni teknolojia iliyobuniwa na kampuni ya Index Lab ili kutoa elimu na ushauri kwa vijana kuhusu afya ya uzazi na jinsia ili kupambana na mimba za utotoni kupitia Facebook Messanger.

Shangazi huyo roboti anapatikana kupitia Facebook Messenger kwa wale wanaomiliki simu janja (smartphones) na hujibu maswali papo kwa papo. Picha|eshangazi
Ingawa chatboat ya kwanza ilitengenezwa mwaka 1950 na mtaalamu wa kompyuta kutoka Uingereza, Alan Turing lakini ilianza kutumika zaidi mwaka  2014 na kuleta mapinduzi ya teknolojia ya mawasiliano duniani.Â
Â