Brela yatoa siku 90 kampuni, biashara kuhuisha taarifa mtandaoni

October 15, 2019 2:33 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Zoezi hilo linahusu biashara na makampuni yaliyosajiliwa nje ya mfumo wa kielektroniki.
  • Mchakato huo unatakiwa kufanyika ndani ya siku 90 kuanzia Septemba 27. 
  • Kampuni zimetakiwa kujaza taarifa za ukweli ili kuepuka hatua za kisheria.

Dar es Salaam. Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) imetoa siku 90 kwa makampuni na biashara zilizosajiliwa nje ya mfumo wa kielektroniki unaotumika sasa kuuhuisha taarifa zao kabla ya muda huo kumalizika. 

May 10, 2018, wakala huo ulizindua mfumo wa kielektroniki wa usajili wa kampuni na biashara na huduma nyingine ikiwemo nembo ya biashara, bidhaa au huduma pamoja na utoaji wa leseni mbalimbali. 

Brela imesema katika taarifa yake kwa umma iliyotolewa Septemba 27, 2019 kuwa huo ni muendelezo wa uhuishwaji wa taarifa za makampuni na majina ya biashara ili kuhakikisha taarifa hizo zinakuwepo katika mfumo wa kielektroniki.

Uhuishaji wa taarifa hizo unafanyika kwa siku 90 tangu ilipotolewa taarifa Septemba 27 mwaka huu.

Katika uhuishaji huo, yapo mambo ya muhimu ya kuzingatia ikiwemo kuwa na namba ya kitambulisho cha utaifa (NIDA) na namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN)

Pamoja na hayo, muombaji anatakiwa kupitia taarifa za kampuni na kuhakikisha zipo sahihi kisheria na kikanuni  pamoja na kujaza fomu katika mfumo wa kielektroniki wa ORS (Online Registration System) na kupakia taarifa zote zinazohitajika zikiwemo taarifa ya mwaka (Annual Returns), mabadiliko yaliyotokea katika kampuni ambayo hayakuwasilishwa awali.


Zinazohusiana


Muombaji pia anatakiwa kuhakikisha kuweka saini kwenye fomu zote ikiwemo na kisha kuzipakia kwenye akaunti na kuzitazama Brela kwa njia ya mtandao.

“Baada ya kukamilisha kuhuisha (Updated) taarifa itahakikiwa na kupatiwa ankara ya malipo na muombaji atatakiwa kulipia benki au kwa njia ya simu,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Msisitizo uliotolewa na Brela ni pamoja na kuwasilisha taarifa sahihi zinazoendana na taarifa zilizopo masijala ya usajili, kufanya zoezi kwa ueledi na ikibidi kuhusisha watu wenye uelewa wa sheria za usajili, kuwasilisha taarifa kamili na kuzingatia maelekezo ya marekebisho kwenye maombi yanayorudishwa.

Pia wahusika wametakiwa kuambatanisha nyaraka sahihi kwa kampuni zenye mabadiliko na kutokurudia makosa na kutoa taarifa za ukweli.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV