Bila kuchelewesha: Magufuli awateua vigogo wa juu Airtel Tanzania

June 12, 2019 9:30 am · Nuzulack Dausen
Share
Tweet
Copy Link

Dk Omari Nundu aliyeteuliwa na Rais John Magufuli kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Airtel Tanzania. Picha|Mtandao.


  • Ni Mwenyekiti na wajumbe wawili wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni hiyo.
  • Mohammed Mtonga awa mwenyekiti mpya wa bodi ya TTCL kumrithi Dk Omari Nundu anayeenda bodi ya Airtel Tanzania.

Dar es Salaam. Siku moja baada ya Bharti Airtel kuanza kutekeleza sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa na Serikali juu ya umiliki wa kampuni ya huduma za simu za mkononi ya Airtel Tanzania, Rais John Magufuli amewateua vigogo wanne kushika nafasi za juu za bodi na menejimenti katika kampuni hiyo ya tatu kwa ukubwa nchini.

Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu iliyotolewa leo (Juni 12, 2019) inaeleza kuwa Rais Magufuli amemteua Dk Omari Nundu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Airtel Tanzania pamoja na wajumbe wawili wa bodi hiyo ambao ni John Sausi na Lekinyi Mollel.

 “Uteuzi wa Dk Omari Rashid Nundu katika nafasi hiyo unatokana na makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya Bharti Airtel International juu ya uendeshaji wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania ambapo mwenyekiti wa bodi anapaswa kuteuliwa na Serikali ya Tanzania,” inaeleza taarifa kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa.

Kabla ya uteuzi huo, Dk Nundu alikuwa ni Mwenyekiti wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na ndiye aliyekuwa miongoni mwa vinara walioeleza namna udanganyifu ulivyofanyika kuipunja Serikali katika mchakato wa ubinafsishaji wa kampuni hiyo ya Airtel.

Ili kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Dk Nundu TTCL, Rais Magufuli amemteua Mohammed Mtonga kuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa shirika hilo lililokuwa na asilimia mbili ya wateja milioni 43.62 wa huduma za simu nchini hadi Desemba 2018.

Mtonga ni Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali katika Wizara ya Fedha na Mipango.


Soma zaidi:


Mbali na kuwateua mwenyekiti na wajumbe wa bodi wa Airtel Tanzania, Msigwa amesema Rais Magufuli kamteua Dk Prosper Mafole kuwa Ofisa Mkuu wa Ufundi (CTO) wa Airtel Tanzania ikiwa ni sehemu pia ya kutekeleza makubaliano na Bharti Airtel.

Bharti Airtel waliingia katika mgogoro na Serikali baada ya kubainika kuwa mchakato wa ubinafsishaji wa Airtel Tanzania hapo awali uligubikwa na udanganyifu jambo lililomfanya Rais Magufuli kutangaza mwaka 2017 kuwa kampuni ilikuwa ni mali halali ya TTCL.

Hata hivyo, baada ya majadiliano ya awamu tano kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Profesa Palamagamba Kabudi, Serikali ilifikia makubaliano na kampuni ya Bharti Airtel yakiwemo kutoa malipo maalum ya Sh1 bilioni kila mwezi kwa miaka mitano, kubadili muundo wa bodi na menejimenti na kuongeza umiliki wa Serikali kutoka asilimia 40 hadi 49 bila malipo yeyote.

Katika hafla ya makabidhiano ya Sh3 bilioni za malipo maalum ya miezi mitatu ya awali kuanzia Aprili 2019, Mwenyekiti Mtendaji wa Bharti Airtel alieleza kuwa makubaliano hayo ni ya kihistoria na kwamba katika nafasi saba za bodi ya wakurugenzi wa Airtel.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV