Amazon yafanya maamuzi magumu uuzaji bidhaa mtandaoni

September 28, 2022 8:30 am · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Imepanga kutoa punguzo kubwa la bei Oktoba 11 na 12, 2022.
  • Siku hizo mbili, bidhaa katika jukwaa hilo zitauzwa kwa bei ya chini isivyo kawaida.
  • Watakaofadika ni watakaonunua fenicha na vifaa vya kielektroniki.

Dar es Salaam. Fursa kwa wale wanaotafuta punguzo kubwa la bei ya fenicha na vifaa vya nyumbani imekaribia kutoka Amazon mapema mwezi ujao kupitia bonanza la mauzo la kampuni hiyo ya biashara ya uagizaji bidhaa mtandaoni. 

Kampuni hiyo ya Amazon imeandaa bonanza la mauzo kwa mara ya pili ndani ya mwaka huu lijulikanalo kama ‘Prime Early Access Sale 2022’, litakaloanza Oktoba 11 hadi 12, 2022.

“Tukio hilo liko wazi tu kwa wanachama wa programu ya Usajili Mkuu wa Amazon (Prime Subscription), na litaangazia “mamia ya maelfu” ya mikataba ya likizo,” amesema Jamil Ghani, makamu wa rais wa Prime, katika mahojiano.

Tukio hilo la mauzo ya siku mbili litatoa ofa nyingi kuhusu vifaa vya kielektroniki zikiwemo runinga, redio,  vihifadhi data (SSD) ili kuwawezesha wananunuzi kuokoa kiasi kikubwa cha fedha.

Amazon imetoa ofa hiyo ya punguzo la bei kwa bidhaa zake ikiwa ni mkakati wake wa kuwashawishi watu kununua bidhaa ikizingatiwa kuwa manunuzi katika jukwaa hilo siyo ya kuridhisha katika kipindi hiki ambacho watu wengi wanakabiliwa na changamoto za kiuchumi.

Pia ni kuwaandaa wateja wake na msimu wa siku za mwisho wa mwaka ili kuwapatie bidhaa zitakazokidhi mahitaji yao kwa bei nafuu. 

Ili kufaidika na ofa hiyo ni lazima uwe mwanachama wa Amazon Prime, usajili unaogharimu Sh324,000 kwa mwaka ambao utakufaidisha kwa huduma ya usafirishaji wa siku mbili bila malipo kwa manunuzi utakayofanya, pamoja na ofa mbalimbali za matangazo.

Habari njema ni kwamba hauitaji kulipia uanachama papo hapo ikiwa unataka tu muda wa kutosha kuchukua fursa ya ununuzi wa kila mwaka wa Amazon.   


Soma zaidi

Unaweza kupata uanachama wa muda mfupi wa Prime ili kukuongezea pesa kwa akiba ya manunuzi kwa njia mbili.

Njia ya kwanza ni Jaribio la kawaida la siku 30 bila malipo, Ikiwa hujawahi kujaribu kutumia Amazon Prime au kutoitumia kwa muda mrefu, unaweza kujaribu kuitumia kwa siku 30 kuagiza bidhaa zako.

Njia ya pili ni kwa mwanafunzi ambao watapata fursa ya kutumia jukwaa hilo kwa miezi 6, baada ya muda huo kuisha akaunti ya usajili huu itatozwa nusu ya gharama ya kawaida ya uanachama wa Prime.

Kuna njia nyingine za kupata Prime bure pia, japokuwa sio moja kwa moja. Unaweza, kwa mfano, kufungua akaunti mpya ukitumia anwani tofauti ya barua pepe, kisha ujaribu Prime kwenye akaunti hiyo mpya.

Unaweza pia kujiandikisha kwenye Prime kwa kutuma maombi kwa kadi ya Visa ya Amazon Prime Rewards, ambayo hukupa asilimia 5 ya pesa taslimu kwenye ununuzi wa vyakula asilia.

Miongoni mwa bidhaa adhimu zinazoweza kupatikana kwa ofa hiyo ni vifaa vya masikioni vya Beats Fit Pro, toleo la 7 la Saa janja za Apple, TV janja za Samsung nchi 55, TV janja za Apple 2021, fenicha na vyakula.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW