Mfumuko wa bei washuka kwa 0.1%, usafiri pasua kichwa

November 9, 2026 5:16 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pungufu kidogo ya kilele cha asilimia 4.3 kilichorekodiwa Agosti na Septemba ambacho ni kiwango cha juu zaidi kuwahi kurekodiwa ndani ya miezi 40 tangu Aprili 2023.

Dar es Salaam. Mfumuko wa bei nchini umepungua kidogo hadi asilimia 4.2 kwa mwaka ulioishia Oktoba 2026 kutoka asilimia 4.3 iliyorekodiwa Septemba mwaka huu, huku gharama za usafiri zikiendelea kupaa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) iliyotolewa Novemba 9, 2026, kushuka huko kunasababishwa na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula. 

“Mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi umepungua kwa asilimia 0.3 kutoka asilimia 3.9 kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2026, huku mfumuko wa bei ambao haujumuishi bidhaa hizo ukipungua kwa asilimia 0.1 katika kipindi sawa na hicho” imesema taarifa ya NBS.

Mfumuko wa bei ni hali ya kupanda kwa bei za huduma na bidhaa katika uchumi kwa kipindi fulani.

Kwa lugha rahisi, ni hali ambayo fedha ile ile ambayo mwananchi aliweza kununua kiasi fulani cha bidhaa, inanunua bidhaa nyingi au chache zaidi kulinganisha na awali.

Hivyo, kupungua kwa asilimia 0.1 ina maana kuwa kasi ya ongezeko la jumla la bei za bidhaa na huduma zinazotumiwa na kaya nchini imepungua kidogo, ingawa bei za baadhi ya bidhaa bado ziko juu ikilinganishwa na mwezi uliopita.

Hata hivyo, kiwango cha asilimia 4.2 kilichorekodiwa Oktoba ni pungufu kidogo ya kilele cha asilimia 4.3 kilichorekodiwa Agosti na Septemba ambacho ni kiwango cha juu zaidi kuwahi kurekodiwa ndani ya miezi 40 tangu Aprili 2023.

Usafiri bado kashehe

Licha ya kupungua kwa mfumuko wa bei wa jumla, usafiri umeendelea kuwa kundi lenye ongezeko kubwa zaidi la bei kwa mwaka, ambapo mfumuko wake umefikia asilimia 14.9 Oktoba 2026, kutoka asilimia 14.0 iliyorekodiwa Septemba mwaka huu.

Takwimu hizo zinaonesha kuwa kasi ya ongezeko la bei katika kundi la usafiri imeongezeka kwa asilimia 0.9 ndani ya mwezi mmoja, hali inayoendelea kuweka shinikizo kwa gharama za usafiri zinazotumiwa na wananchi na shughuli za kiuchumi.

Kwa mwezi Novemba mwaka huu, bei ya rejareja za petroli na dizeli iliongezeka hadi Sh4,083 na Sh4,057 kwa lita, mtawalia, ikiwa ni viwango vya juu zaidi kurekodiwa ndani ya miaka mitatu iliyopita.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), ongezeko hilo limechagizwa na kuendelea kwa mgogoro wa Mashariki ya Kati, ambako Tanzania hununua sehemu kubwa ya mafuta yake. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
9 Nov, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
9 Nov, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Lissu kukosa sifa za kugombea 2030?

Lissu kukosa sifa za kugombea 2030?

Nukta TV

BEI YA MAFUTA DAR | Sh10,000 kununua lita 2.44 za petroli, 2.42 za dizeli

BEI YA MAFUTA DAR | Sh10,000 kununua lita 2.44 za petroli, 2.42 za dizeli

Nukta TV

Namna Rais Samia alivyoshiriki kwenye Uchaguzi Mdogo, Jimbo la Chamwino

Namna Rais Samia alivyoshiriki kwenye Uchaguzi Mdogo, Jimbo la Chamwino

Nukta TV