Brenda Msangi kung’atuka CCBRT Machi 2027

July 21, 2026 1:01 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni baada ya kuitumikia CCBRT kwa miaka 17, na miaka 8 kama Mkurugenzi Mtendaji.
  • Atang’atuka wakati ambao CCBRT ipo kwenye hatua muhimu ya kuimarisha uendelevu wa taasisi na upanuzi wa huduma.

Dar es Salaam. Bodi ya Wakurugenzi ya Hospitali ya CCBRT imetangaza kumpa mkono wa kwaheri Mkurugenzi Mtendaji wa  hospitali hiyo Brenda Msangi ifikapo Machi 31, 2027.

Taarifa ya Dk Redempta Mbatia, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi CCBRT iliyotolewa Julai 20, 2026 inabainisha kuwa uamuzi huo ni sehemu ya mchakato wa muda mrefu wa hospitali hiyo.

“Mabadiliko haya ya uongozi ni sehemu ya mchakato uliopangwa wa kurithi uongozi ambao bodi imekuwa ikiutayarisha kwa muda wa miezi 18,” amesema Mbatia.

Brenda aliyeitumikia CCBRT kwa zaidi ya miaka 17 alikuwa Mtanzania na mwanamke wa kwanza kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Desemba 2018 wakati ikiwa katika kipindi cha mageuzi ya huduma zake za afya.

Mwanamama huyo atang’atuka katika nafasi hiyo wakati ambapo CCBRT ipo kwenye hatua muhimu ya kuimarisha uendelevu wa taasisi, kupanua huduma zake na kuongeza uwezo wa kuwafikia wananchi wengi zaidi.

Kwa mujibu wa Mbatia, bodi itaanza mchakato wa kumpata Mkurugenzi Mtendaji ajaye, huku Brenda akiendelea kuiongoza CCBRT hadi Machi 31, 2027 na kushirikiana na bodi kuhakikisha mabadiliko ya uongozi yanafanyika kwa utaratibu maalum.

CCBRT pia hutoa huduma kwa watoto wenye ulemavu na changamoto mbalimbali za kiafya, ikiwemo utindio wa ubongo.Picha|CCBRT.

Brenda Msangi ni nani?

Brenda Msangi ni mmoja wa viongozi wanawake wanaotajwa katika mageuzi ya sekta ya afya nchini Tanzania, akiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika uongozi wa taasisi za afya, dawa na mifumo Afrika na Ulaya. 

Alizaliwa na kukulia mkoani Dar es Salaam  ambapo alianza safari yake ya elimu katika Shule ya Msingi Oysterbay kabla ya kujiunga na Shule ya Sekondari ya Wasichana Jangwani kwa ngazi zote mbili za elimu ya sekondari.

Akiwa mwanafunzi wa kidato cha tano na sita alisoma mchepuo wa sayansi (PCB), lakini ndoto yake ilielekezwa zaidi kwenye taaluma ya famasia badala ya udaktari. 

Baadaye alijiunga na ngazi za juu za elimu  nchini Uingereza ambako alipata Shahada ya Uzamili ya Famasia kutoka Chuo Kikuu cha Brighton na baadaye Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Biashara katika Sekta ya Afya (MBA Healthcare) kutoka Chuo Kikuu cha Plymouth na baadae kupata mafunzo ya uongozi wa bodi kutoka Harvard Business School Executive Education.

Baada ya masomo, Brenda alianza safari yake ya kitaaluma katika sekta ya afya nchini Uingereza, ambako alipata nafasi ya kusimamia timu katika sekta ya famasia. 

Mwaka 2009 alirejea Tanzania na kujiunga na CCBRT kama Naibu Mkurugenzi wa Programu za Jamii, nafasi iliyompa uzoefu mkubwa katika usimamizi wa huduma za afya na maendeleo ya jamii. 

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa CCBRT Brenda Msangi (Kulia) Mkuu wa Idara ya Mifupa na Utengamao CCBRT Dkt. Luijisyo Mwakalukwa (katikati) na Wataalamu wengine wa matibabu ya Mguu Kifundo hospitalini hapa wakikata keki na mmoja wa watoto aliyetibiwa na kupona ulemavu huo. Kila mwaka 3 Juni, 2021 duniani.Picha|CCBRT.

Baadaye alipanda ngazi na kuwa Afisa Mkuu wa Uendeshaji (Chief Operating Officer) kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa CCBRT Desemba 2018.

Akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa CCBRT, Brenda ameongoza taasisi hiyo katika kipindi cha mageuzi yaliyolenga kuimarisha uendelevu wa kifedha, kuboresha mifumo ya utoaji huduma na kupanua ushirikiano kati ya Serikali, wafadhili na sekta binafsi. 

Chini ya uongozi wake, CCBRT imeendelea kuwa miongoni mwa taasisi kubwa za afya nchini zinazotoa huduma za matibabu na urekebishaji wa viungo kwa jamii zenye uhitaji.

Mbali na nafasi yake CCBRT, Brenda amekuwa akihudumu katika bodi mbalimbali zikiwemo CEO Roundtable of Tanzania, World Vision Tanzania na taasisi nyingine, akijikita katika masuala ya utawala bora, usimamizi wa hatari, maendeleo ya rasilimali watu na uendelevu wa taasisi. 

Pia ni mwanzilishi wa jukwaa la ‘Dear Girl Child BMK’ linalolenga kuwawezesha wasichana na wanawake katika uongozi na kujenga kujiamini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
21 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
21 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Prof. Mbalawa, Waziri Misri wavutana, makubaliano ujenzi Bandari ya Bagamoyo

Prof. Mbalawa, Waziri Misri wavutana, makubaliano ujenzi Bandari ya Bagamoyo

Nukta TV

Rais Samia: Nchi za Afrika zinaweza, bila ushiriki wa mataifa ya nje

Rais Samia: Nchi za Afrika zinaweza, bila ushiriki wa mataifa ya nje

Nukta TV

Mfahamu ‘African Goose’ bata mwenye kilo 14 anayeuzwa Sh2 milioni

Mfahamu ‘African Goose’ bata mwenye kilo 14 anayeuzwa Sh2 milioni

Nukta TV