Mchemsho wa nyama na viazi kwa kutumia ‘pressure cooker’

July 28, 2023 11:33 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Hutumia umeme kidogo kuivisha chakula kwa haraka
  • Ina uwezo wa kupika aina nyingi ya vyakula kwa muda mchache.

‘Pressure cooker’ ni moja ya kifaa kinachotumika kwa ajili ya mapishi ya aina mbalimbali majumbani, migahawani pamoja na hotelini.

Wengine hupenda kuiita sufuria ya umeme, sifa kubwa ni uwezo wake wa kuivisha chakula kwa muda mfupi zaidi tofauti na kutumia sufuria za kawaida.

Mathalani, kama mtu hutumia saa moja kuivisha maharage kwa kutumia jiko na sufuria ya kawaida, basi kwa kutumia pressure cooker unaweza kutumia nusu ya huo muda au chini ya hapo.

Kifaa hicho cha mapishi kinachozidi kupata umaarufu kwa siku za hivi karibuni kinaweza kupika aina mbalimbali za vyakula ikiwemo vya vya nafaka kama maharage, aina mbalimbali za nyama na mboga za majani.

Ina faida kiafya.

Mgandamizo wa hewa (pressure) unaozalishwa na kifaa hicho huwezesha vyakula kuiva kwa haraka bila kupoteza virutubisho vya chakula husika  kulinganisha aina nyingine ya kifaa cha umeme.

“Mvuke uliogandamizwa husaidia kutunza virutubisho vyote, utafurahia chakula chenye virutubisho na afya,” inasema tovuti ya kampuni ya Dessin ambayo huuza vifaa hivyo.

Baada ya kufahamu faida za kiafya za kutumia ‘pressure cooker’, fuatana nami ujifunze namna rahisi  ya kutumia kifaa hicho kupika mchemsho wa  nyama ya ng’ombe na viazi mviringo.

Mbali na viazi na nyama, unaweza pia kutumia ‘pressure cooker’ kupika wali, pilau pamoja na vyakula vingine.Picha|Simplician.

Maandalizi

Hakikisha ‘pressure cooker’ yako ni safi, imekaushwa maji tayari kwa kuanza mapishi. Andaa nyama, viazi, hoho, karoti, kitunguu kisha uoshee na ukate kwa saizi upendayo.

Baada ya maandalizi hayo chomeka waya wa pressure cooker kwenye umeme, wakati inawaka anza kwa kuweka nyama, tangawizi na kitunguu swaumu katika sufuria ya pressure cooker kisha mimina maji ya kulingana na wingi wa nyama na ufunike ili hewa isiingie

Kama viazi vyako ni vingi kuliko nyama au ni vigumu kuiva unaweza kuweka kuviweka wakati huu viive pamoja na nyama na kama sio vingi basi unaweza kuviweka wakati wa kuunga.

Hatua inayofuata ni kuweka muda, pressure cooker aina nyingi huwa na sehemu maalum inayoonesha aina ya chakula pamoja na muda utakaotumika kuivisha chakula hicho.

Mathalani mapishi ya nyama ambayo tutaandaa leo huhitaji dakika 25 mpaka dakika 45 kulingana na wingi wake.

Baada ya kuweka muda bonyeza kitufe kitakachoruhusu kuanza kwa mapishi yako. Subiri baada ya mpaka muda uishe ili uweke viiungo.

Ukihakikisha nyama na viazi vimeiva ongeza hoho,nyanya ya pakti au ya kusaga kama unapendelea, karoti, kitunguu, chumvi na viungo vya mchuzi kisha subiri kwa dakika nyingine mbili.

Baada ya hapo mchemsho wako utakuwa tayari kwa kuliwa.

Jipange

Pamoja na kuivisha chakula kwa haraka lazima utahitaji nishati ya umeme, hivyo walioko katika maeneo yasiyo na huduma hiyo wanaweza kupata changamoto.

Blogu ya ‘let’s save electricity’ inayojihusisha na kupima matumizi ya umeme inasema kila ‘pressure cooker huwa na kiwango tofauti na matumizi ya umeme kutokana na ukubwa na jinsi iliyotengenezwa.

“Pressure cooker nyingi zenye Wati kuanzia 700 mpaka 1,200 hutumia hadi uniti 18 kwa mwezi kama ikitumiwa kila siku kwa muda wa dakika 30,” imesema Blogu hiyo.

Unasubiri nini? jipatie ‘Westpoint pressure cooker’ yako sasa kwa punguzo la bei la Sh130,000 tupigie simu kwa namba 0677 088 088 au kupitia tovuti yetu www.jikopoint.co.tz.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
12 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV