Wafahamu wabunge 8 waliotemwa katika baraza la mawaziri Tanzania

November 17, 2025 6:54 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja na Dk Dotto Biteko, Hussein Bashe na Jenista Mhagama.
  • Mawaziri wateule wataapishwa kesho Novemba 18, 2025.

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza baraza jipya la mawaziri watakaoratibu shughuli za Serikali katika miaka mitano ijayo akiwatema mawaziri nane waliohudumu katika baraza la mawaziri lililopita.

Rais Samia ametangaza majina hayo ya baraza jipya leo Novemba 17, 2025 alipokuwa akizungumza na wanahabari Chamwino Dodoma ikiwa ni muendelezo wa kupanga safu mpya ya awamu ya pili ya uongozi wake.

“Tumeitana tuzungumze mustakabali wa Serikali na Taifa letu, juzi nikizungumza na Bunge nilisema sitachukua muda mrefu nitaunda na baraza la mawaziri hivyo ujio wangu hapa ni kuwataja wale watakao tusaidia kwenye kazi hizo za mawaziri na manaibu mawaziri,” amesema Rais Samia.

Katika orodha hiyo Rais Samia amewataja mawaziri 27 pamoja na manaibu waziri watakaohuduumu katika wizara hizo akiwatema wengine saba akiwemo Dotto Mashaka Biteko aliyekuwa Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu tangu alipoteuliwa Agosti 2023.

Nyota ya Biteko ambae pia ni mbunge wa jimbo la Bukombe(CCM) katika mkoa wa Geita kaskazini magharibi mwa Tanzania kuanzia mwaka 2015 ilianza kungaa mwaka Januri 9, 2018 alipoteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nishati na mwaka mmoja baadae kupandishwa cheo kuwa Waziri wa Wizara hiyo aliyoiongoza hadi mwisho wa awamu iliyopita..

Kwa sasa wizara hiyo itaongozwa na Deogratius Ndejembi, mbunge wa jimbo la Chamwino (CCM), huku Naibu Waziri akiwa ni Salome Makamba, Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga (CCM).

Hussein Bashe

Kwa mara  ya kwanza tangu mwaka 2022 Wizara ya Kilimo imepata waziri mpya mara baada ya Rais Samia kumtema Hussein Bashe  na kumteua Daniel Chongolo kuiongoza wizara hiyo.

Bashe ambaye ni mbunge wa Nzega mjini (CCM) aliialianza kuitumikia jimbo hilo mwaka 2015 na baadae kuitumikia Wizara ya Kilimo kama Naibu Waziri hadi kuwa Waziri kamili.

Jenista Mhagama

Jenista ni miongoni mwa wabunge wakongwe ambapo alingia bungeni mwaka 2005, na tangu wakati huo amehudumu katika nafasi mbalimbali za uongozi Serikalini kuanzia kuwa Naibu Waziri wa Elimu hadi kuwa Waziri katika  Ofisi ya Waziri Mkuu akisimamia sera, Bunge, ajira na masuala ya watu wenye ulemavu. 

Mwaka 2022 aliteuliwa kuongoza Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), na mwaka 2024 akahamishiwa Wizara ya Afya. Licha ya kuchaguliwa tena kuwa mbunge katika jimbo la Peramiho, Mhagama hajaingia katika orodha mpya ya baraza la mawaziri.

Innocent Bashungwa

Unaweza kusema nyota ya uwaziri imeota manyoya katika awamu ya pili ya uongozi wa Rais Samia baada ya jina lake kutokutokea katika orodha hiyo mpya ya baraza la mawaziri licha ya kuhuduumu kwa zaidi ya miongo miwili tangu mwaka 2015.

Kwa sasa nafasi ya Bashungwa aliyehudumu katika jumla ya wizara nne ikiwemo ya mwisho ya Mambo ya Ndani ya Nchi  inashikiliwa na George Simbachawene.

Stergomena Tax

Dk Stagomena ni miongoni mwa wabunge wachache wanawake waliong’ara mwanzoni kabisa mwa uongozi wa Rais Samia ambapo muda mchache baadae aliteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kuanzia 30 Agosti 2023 Sasa.

Hata hivyo Rais Samia amelitema jina na mwanamke huyo na Rhimo Nyansaho kuchukua nafasi yake.

Sulemani Jaffo

Selemani Jafo ni Mbunge wa Kisarawe tangu mwaka 2010 akihudumu katika nafasi mbalimbali za uwaziri ikiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira). 

Mara ya mwisho alihudumu kama Waziri wa Viwanda na Biashara, nafasi ambapo kwa sasa inashikiliwa na Judith Kapinga.

Pindi Chana

Pindi Hazara Chana ni mbunge wa viti maalum tangu 2010 akihudumu katika wizara tatu  tofauti tangu mwaka 2022 ikiwemo Wizara ya  Maliasili na Utalii, Utamaduni, Sanaa na Michezo, na tangu 1 Septemba 2023 ni Waziri wa Katiba na Mambo ya Sheria nafasi ambay kwa sasa imechukuliwa na 

Damas Daniel Ndumbaro 

Ndumbaro ambaye pia ni mbunge wa Songea Mjini (CCM) amehudumu katika nafasi mbalimbali za uwaziri Waziri wa Maliasili  na Utalii, baadaye Waziri wa Katiba na Sheria, pamoja na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. 

Kwa sasa nafasi ya Ndumbaro inashikiliwa na Juma Homera.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...

Enable Notifications OK No thanks